Showing posts with label ENTERTAINMENT. Show all posts
Showing posts with label ENTERTAINMENT. Show all posts

Thursday 25 October 2018

JE UNATAKA KUJIUNGA NA 1XBET? NI RAISI SANA NJOO UFUATE MAELEKEZO KWA UMAKINI UWEZEKE KUVUNA PESA

Sunday 9 September 2018

MOVIE| JIG SAW -2018movie • DOWNLOAD FREE


DOWNLOAD AND SHARE



General Information
  • Title: SAW (JIGSAW)
  • Director: The Spierig Brothers
  • Producer: Gregg Hoffman
  •  Country: US
  • Time: 92 Minutes

PLOT
Baada ya kufuatilia mfululizo wa movie kali za Saw, mwaka jana wamerudi tena na hii inaitwa JigSaw, mara ya mwisho Mtaalam John Kramer alionekana amekufa, Lakini leo hii hapa mchezo wa mauaji umerudi tena baada ya watu watano Mitch, Anna, Ryan, Carly, na mwanaume mmoja ambae hajajulikana kutokana na kupoteza fahamu, wanatakiwa kutubu dhambi zao la sivyo wanauwawa

CHEK KIONJO





Saturday 9 June 2018

ASLAY:- NYIMBO YA NINOGESHE NI YANGU MIMI NANDY KAPEWA TU

Mwanamuziki Aslay amefunguka na kusema kuwa wimbo aliimba Nandy wa ninogeshe ambao umefanya vizuri tangu umetoka katika station mbalimbali aliuandika yeye na alitakiwa kuutoa siku nyingi lakini ilibdi apewe Nandy .

Aslay anasema kuwa nandy alikuwa hana wimbo wa kutoa kwa kipindi hicho hivyo ikabidi wimbo uliokuwa tayari ulioandikwa na aslay apewe Nandy kama menejiment iliyokuwa imepanga na kuona kuwa itakuwa sahihi.


Hata Nandy pia alishawahi kusema katika moja ya mahijiano yake ya nchini Kenya hivi karibuni kuwa wimbo huo uliimbwa na Aslay

ninogeshe ni wimbo ambao nilitakiwa kuuimba nikiwa na nandy , ila kwa sababu nandy hakuwa na wimbo kwa kipindi hicho ilibidi menejiment iamue kupewa nandy aimbe peke yake.

T I D:- AIBUKA NA POVU KWA MEDIA ZA BONGO

Msanii TID amesema kuwa utaratibu wa wadau/media kushusha wasanii pale wanapodai maslai yao na kuwapandisha wengine ndio kitu kinaathiri muziki wa Bongo Flava.
Muimbaji huyo ameeleza kuwa kitu hicho ndicho kilitokea kwenye muziki wake na kwa sasa kimemtokea Diamond.

“Na kweli anaweza because he has a media, yaani yeye ndio kama Mungu anajiona but mimi hapana. Nilifanya kosa hilo lakini kosa hilo ndilo limewasanua wasanii wengine, unaona msanii kama Diamond naye amekataa,” amesema.

“So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa tunamleta Diamond tukushushe wewe. At the end Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani,” TID ameiambia Wasafi TV.

TID ameongeza kuwa hajaona kitu kama hicho nchini Kenya kwani bado anamuona Jaguar ni msanii mkubwa, Nonini ni msanii mkubwa anapewa heshima yake hakuna underground yeyote amewekwa pale kumshusha Nonini.

Thursday 7 June 2018

OMMY DIMPOZI:- WCB KUNA NYIMBO MBILI TU KARI

Msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz ametaja nyimbo mbili kutoka label ya WCB ambazo anaona zinafanya vizuri.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Wanje’ ametaja ngoma ngoma hizo kuwa ni Kwa Ngwaru ya Harmonize na Pochi Nene ya Rayvanny.

“Moja wapo ni hiyo kama unavyosema Kwa Ngwaru ni wimbo ambao unafanya vizuri, yeah!, kuna mwingine nimesikia wa Rayvanny Pochi Nene, kwa hiyo kwa currently ni nyimbo ambazo naweza kusema zinafanya vizuri,” Dimpoz ameiambia Citizen Radio.

Katika hatua nyingine amefunguka ni lini hasa bifu lake na Diamond litaisha kwa kusema; “Kila jambo lina wakati wake kwa hiyo time itakapofika mambo yote yatakaa sawa, tuombe Mungu".

JACLINE WOLPER:- HARMONIZE NI TAPERI MUSIKUBARI KUTAPERIWA

Mwanadada Wolper ameamua kumlipua harmonize na kumwita tapeli baada ya harmonize kutangaza katika vyombo vyahabari kuwa kutakuwa na show yake mbagala na katika show hiyoa atakaekuwa aki-host ni hjackline wolper.

Harmonize alitoa taarifa hiyo na kusema kuwa hana bifu na Jacky na kuwa wameamua kuanzia sasa kufanya kazi pamoja ili kuondoka kuwagawa mashabaki. lakini baada ya tangazo hilo la Harmonize, uongozi wa Jacky ulikanusha taarifa hizo na pia Jacky mwenye anmesemakuwa hayupo kabisa tanzania na kwamba wanaofanya na kutangaza hayo ni matapeli sugu.

TANGAZO TANGAZO , NAOMBENI MTAMBU KUWA SIPO TANZANIA NA WALA SITAKUWEPO KABISA KATIKA SHOW YOYOTE, IWE YA MBAGALA AU YA POSTA , MIMI KAMA WOLPER SIHUSIKI…YOTE WANAYOYASEMA NI UONGO NA WALA SIHUSIKI..SITAKI WATU WATUMIE JINA LANGU KUVUTA WATU, EPUKANA NA MATAPELI ..ASANTE SANA…#EPUKAMATAPELISUGU #ACHENIKUTUMIAJINALANGU #SIPOTANZANIANASIRUDIMPA

Sunday 3 June 2018

HARMONIZE :-SIWEZI KUMCHAGULIA MKE WA KUOA DIAMOND AOE YEYOTE


                                                 
 Diamond Platnumz bado amezid kukamata headline mitandaoni kuhusu maisha yake ya kimahusiano, safari hii Harmonize naye katia neno katika hayo yanayoendelea.
Harmonize amesema hawezi kumshauri Diamond Platnumz awe na nani kwa sasa kati ya Zari, Hamisa au Wema ila ataonesha ushirikiano kwa yeyote akayechaguliwa na Diamond.
“Mimi yeyote; akiniambia leo tunarudi South Africa mimi nipo pale Pretoria, akiambia kwa wakati huu tuhamie Unu
nio, nipo pale kwa Madam, akiambia official tunachukua Hamisa tunaweka ndani nipo, sasa jamani kwani utamu napata mimi,” Harmonize ameiambia Wasafi TV.
Awali Harmonize alisema kuwa licha ya kufanya kazi na Diamond kwa ukaribu na kusaidiana katika mambo mbali mbali ni vigumu kwa yeye kumshauri kuhusu mahusiano yake ila watu wa karibu kutoka kwenye familia yake kama Romy Jons na Esma Platnumz wanaweza kufanya hivyo.                         

Saturday 2 June 2018

MOBETO:- DIAMOND NDUGU ZAKO WATANIESHIMU MPAKA NITAKAPO WAFURIA VYUPI

Mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye ni mama mtoto wa Diamond Platinumz amefunguka kupitia ukuraasa wa Instagram wa Baba mtoto wake, Diamond Platinumz mara baada ndugu wa msanii huyo kuongea maneno yaliyoonesha kumkejeli.
Kufuatia maneno hayo ambayo yamezagaa katika mtandao wa Instagram Hamisa ameibuka na kuandika waraka mzito akimtaka Diamond Platinumz kuoa mwanamke ambaye ndugu, maneja na mashabiki wa Diamond wanamtaka aoe kwani katika andiko lake ameonesha kukerwa na baadhi ya maneno yaliyoongelewa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye mara baada ya wimbo wa Iyena kutoka.
Ambapo katika wimbo huo Diamond ameonekana akifunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake Zarinah Hassan.
Ndo uoe Huyo Mwanamke ambae anatakiwa na Ndugu zako … na manager zako bila kusahau mashabiki … sio kutwa mie mtoto wa watu naandamwa na kukaliwa mie kooni!!! Sijakuita wala kukufunga kamba ……
Kila siku maneno mimi Kwani alishindwa kukufata kukushauri ? Mpaka akimbilie kwenye MaTv na Mitandao ? Unapokaa hapajui , number ya simu yako pia hana? …. kwani mie hayo maTv hayaombi kuniombi kunihoji mbona nakaa kimya ? Tena saa ingine nakaa Kimya kuwastiri kwa mengi na pia dee akikua asione hii migogoro lakin ndugu zako hawabebeki its too much 🙌🏽 talk to Your familia maana wewe ni mwananume na uwezo wa kuyamaliza ………
Na pia waambie unahitaji Mke sio House girl wa Nyumba🤚🏽… Mwanamke kazi yake kukupikia Ule , au nlikua sikupikii tena sio wewe tu na Ndugu zako mkala na kusaza ? … leo imekua hamisa hajui kupika kusafisha nyumba kwahiyo chumba chako tukimaliza lalana huwa anasafisha nani ?
Au walitaka niende kuwafulia vyupi vyao nikimaliza niwapigie deki mpaka chumbani kwao ? Wakishindwa kuniheshimu basi waambie waheshimu damu yako . The End !
Mobeto amefunguka hayo kufuatia post mbalimbali zilizokuwa zikitumwa na watu wa karibu wa Diamond Platinumz wakidai kuwa wamemkumbuka sana Zari hivyo wanataka arudi ili ndoa iweze kufungukika.
Wimbo wa Iyena pamoja na mistari yake umewaibua watu wengi na mashabiki wengi ambao wameonekana kumshambulia kwa maneno mwanadada Hamisa Mobetto.

Monday 28 May 2018

ASLAY :- AFUNGUKA KUACHANA NA MAMA WATOTO WAKE

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amekiri kupigana chini na aliyekuwa mpenzi wake na Mama watoto wake Tessy Chocolate.
Siku chache zilizopita kuna tetesi zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wapendanao hao wameachana baada ya Tessy kufuta Tatoo aliyokuwa amechora jina la Aslay mkononi.
Hatimaye Aslay amethibitisha tetesi hizo Kwenye Interview na Bongo 5 ambapo ameweka wazi kuwa yeye na Tessy wamepigana chini na kila mtu anaendelea na maisha yake.
Ingawa Aslay hajaweka wazi sababu ya kuachana lakini inasemekana kuwa alichepuka kwani Tessy alishawahi kudokeza hilo kwa maneno ya mafumbo aliyoposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ni kweli tumezinguana mimi na mama watoto wangu sahivi kidogo kila mtu anaangalia maisha yake ila mimi na yule ni ndugu tumezaa tuna mtoto wetu tunashukuru mtoto wetu anaendelea vizuri hilo ndo la maana”.

DIAMOND:- SIWEZI KUMUOMBA MSAMAHA ZARI ATA SIKU MOJA

Msanii wa bongo fleva maarufu nchini , Diamond Platinumz kwa mara ya kwanza amefunguka na kuzungumzia swala lake la kuachana na Diamond na kumuomba radhi mwanamama huyo ambapo taarifa za hapo awali ziliwahi kusema kuwa kwa sasa Diamond amekuwa akipiga safari nyingi za Afrika ya Kusini ili kuomba radhi kwa mwanamke huyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari alipoulizwa kuhusu mambo mengi na vijembe vingi ambavyo diamond amekuwa akitupiwa na mwanamama huyo hasa vya hapa karibuni alipokuwa kenya, diamond alisema’ hayo ya kenya bwana tuachane nayo, mimi nadhani yameshapita naomba tuendelee na haya yabsasa itapendeza sana”
Hata hivyo, mwandishi hakuishia hapo ndipo alipoamua kumuuliza moja kwa moja kuhusu yeye kuwa akisafiri kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya kuomba radhi kwa zari huku akienda kwa siri mara kwa mara na diamond alijjibu kuwa safarizake za afrika ya kusini haziusiani na mambo hayo.
Ni muda sasa umepita tangu wawili hao kutengana na kumekuwa na mogogoro mingi kati yao hasa kupitia katika mitandao ya kijamii lakini hii haijamfanya diamond kuacha kuwa na hamu ya watoto wake , mara kwa mara amekuwa akienda kuwaona kama alivyokiri.

ni kweli ninaenda na so mara moja au mara mbili nimekuwa ninaenda,nakwenda kule sio kwa ajili ya kumuomba msamaha , hapana ila ninakwenda kule kwa ajili ya kumuona wanangu tu,haiwezekani niwe ninatuma pesa za matumizi tu alafu ninafka mpaka afrika ya kusini na nisiende kuwaona wanangu.
hao wanaosema kuwa sijui nimekuwa nikimuangukia nadhani yatakuwa ni maoni yao tu wala sio yangu, ni maneno yasiyokuwa na msingi, zari ni mama wa watoto wangu na itabaki kuwa hivyo.

HAMISA MOBETO ATESWA NA KASHIFA YA KUAZIMA NGUO

Mwanamitindo na Muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto amejibu tuhuma alizotupiwa wiki iliyopita kuwa ameazima nguo za mtu na kudanganya za kwake.
Sakata hilo lilianza wik iliyopita baada ya Mobetto kuposti nguo aliyovaa Sarah mpenzi wa Harmonize na kusema imetoka kwake jambo ambalo sio la kweli kwani nguo hiyo iliyengenezwa na mwanadada mwingine anayejiita Ab Desgners ambaye alimwandikia ujumbe mwanamitindo huyo kuwa awe mkweli.

Baada ya maneno kuzuka Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimsaka mwanadada anayeitwa Aliyah ambaye alidai ndio mmiliki halali ambaye alifunguka:
Baada ya Tuhuma hizo Hamisa alifunguka  na kudai kuwa habari hizo ni za uongo na kilichotokea ni kutoelewana

Ni kweli nguo ni zangu kwani Mobeto alikuja kwangu na kunieleza kuwa anataka achukue nguo zangu avae alafu atasema zimetoka kwake ili anitangazie biashara, na kusema kwamba akipata wateja aniletee, mimi nilikataa, nikasema kama anachukua nguo anitangazie kwa jina langu la sivyo nimuazime tu arudishe”.

Jamani mimi nilishaeleza sana na hata nilipoweka kwenye mitandao niliandika kuwa nguo hizo zimebuniwa na yeye sasa mimi nashangaa watu wananichafua kwenye mitandao“.

Sunday 27 May 2018

SHETA AFUNGUKA KUWA HANA BIFU NA DIAMOND




                       

Msanii wa muziki Bongo, Shetta amefunguka kwanini kipindi hiki haonekani karibu na Diamond kama ilivyokuwa mwanzo.
Shetta amesema kwa sasa kinachowatenganisha ni biashara tu na hakuna zaidi ya hapo.
“Sidhani kama kuna bifu lakini mimi nafikiri biashara sababu mwanzo tulikuwa tunaishi kama washikaji lakini ikimbukwe sote ni wanamuziki ili kutafuta inabidi kila mtu apambane,” amesema.

“Siri ya biashara kila mmoja anataka kufanikiwa, kila mmoja anataka kuwa namba moja na kuna series za mafanikio. Automatic wewe kama mwanamuziki na sifaidiki na wewe kwa njia moja au nyingine, siwezi kukupa njia zangu na wewe huwezi kunipa njia zako lakini haiwezi kuwa kama tatizo,” Shetta ameiambia Wasafi TV.

Utakumbuka wawili hawa walishafanya ngoma mbili pamoja ya kwanza ilikwenda kwa jina la Nidanganye na nyingine ni Kerewa zote zikiwa za Shetta.

Thursday 24 May 2018

MTOTO WA STEVEN NYERERE AFANANISHWA NA RICH

Ikiwa leo ni siku ya kuzaliwa na mtoto wa Steve aliyezaa na Matilda Weru Sengo kumezuka mapya atika kurasa mbalimbali za udaku baada ya mtoto huyo kufananishwa na msanii mwingine kutoka Bongo movies Single Mtambalike maarufu kama Richie.

Picha za mtoto huyo zilizosambaa sana katika mitandao ya kijamii huku wengi wakuthibitisha maneno mengi yaliyokuwa yakisemwa na wawili hao kuwa wanakanusha , hatimaye sasa ukweli umegundulika kuwa wawili hao walikuwa wapenzi lakini bado kitendawili kimeshindwa kutatuliwa baada ya watu wa udaku kuanza kumfananisha mtoto huyo na msanii mwenzao wa filamu nchini.

Steve Nyerere na Weru sengo wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu na lakiniwawili hao wamekuwa wakisema kuwa hawapo pamoja lakini kwa sasa wameamua kuthibitisha kwa kuonyesha kuwa wana mtoto na ametimiza umri wa mwaka mmoja sasa.

ESMA :- AMKANA HAMISA MOBETO MCHANA KWEUPE

Mwanadada Esma Platinumz amemkana Hamisa Mobeto kwamba sio rafiki yake tena kwa sasa hivi na kusema kuwa hajui chochote kuhusu mahusiano ya rafiki yake huyo na kaka yake Diamond Platinumz.

Akiongea katika sherehe waliofanya wikiend iliyopita walipokuwa wakiukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani, esma anasema kuwa hajui chochte kuhusu mahusiano ya wawili hao na ndio kwanza ameyasikia kutoka kwa mtangazaji huyo na kama ni kweli basi hana cha kuzungumza kuhusu hilo.
 Ndo kwanza nasikia kwako taarifa hizo wala hata sijui kama wamevalishana pete,hamisa mobeto alikuwa rafiki yangu lakini no comments,alikuwa rafiki yangu lakini sio kwa sasa hivi.

Wednesday 23 May 2018

MAMA DIAMOND :- SIJA MPIGA HAMISA MOBETO NO COMMENT

Mama mzazi wa msanii Diamond Platinumz hivi karibuni amekuwa katika headline karibia kila kona kutokana na skendo iliyokuwa ikisambaa katika mitandao kuhusu yeye kumpa kipigo mwanamke anaesemakana kutoka kimapenzi na mwanae pekee ya kiume Diamond .
Inasemekana kuwa mama Huyo aliamua kumpa kichapo hamisa kutokana na kuwa hapendi Hamisa kuwa karibu na mtoto wake huku akisema kuwa hamisa hana adabu hivyo hafai kabisa kuwa mkwe wake.
Mitandao ya kijamii imekuwa ikiripoti na kumtafuta sana kuzungumzia swala hilo, lakini pia katika mitandao ya kijamii watu wengi wamekuwa wakimtukana mama huyo kwa kuwa amekuwa akijihusisha sana na maswala ya mitandao na hasa kumfatilia sana mtoto wake ambae ndio amekuwa source ya matatizo yote.
Akiwa kama mama na mtu mzima watu wamekuwa wakimtaka mama huyo kauchana na mitandao lakini pia aache kufatilia maisha ya mtoto wake wa kiume.
Sasa mama huyo ameamua kuwajibu wanaomtukana katika mitandao na kusema kuwa hata yeye hapendi kufatiliwa na watu kwa sababu hayo ni maisha yake na familia yake
Waache kufatilia maisha yangu na familia yangu na wao wafatilie familia zao pia,kila mtu 

Waache kufatilia maisha yangu na familia yangu na wao wafatilie familia zao pia,kila mtu anafamilia yake waiache ya kwangu na kuhusu ku-unfollow hicho ni kitu cha kawaida wenyewe tushazoea.

SHILOLE :- AWATAKA WASANII WA KIKE KUOLEWA NA SIO KUJIANGAISHA


Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewataka wasanii wenzake wa kike Kuolewa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili waache kufanya zinaa.

Shilole ambaye alifunga ndoa na mume wake Ashraf Uchebe mwaka jana mwishoni ameonekana kifurahia ndoa hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Shilole amekiri kuwa katika mfungo wa mwaka huu, anaona raha mno kwani ndiyo kwa mara ya kwanza umemkuta ndani ya ndoa na amekuwa akifunga na kufanya dua na mumewe tofauti na miaka mingine ambayo alikuwa hajaolewa, alikuwa akilegalega kufanya sala na kufunga.

"Huu ni mfungo wa kipekee kwangu kwani ndiyo kwanza umenikuta ndani ya ndoa, kiukweli ninajisikia raha mno ambayo sikuwahi kuipata awali".

Lakini pia Shilole aliwataka mastaa wa kike ambao hawajaolewa wajitahidi waolewe na waachane na kuzini kwa sababu dua zao ndipo zitakapopokelewa pia anawaombea ili wapate waume wema kama yeye alivyopata mume mwema anayemuongoza katika njia nzuri ya kumjua zaidi Mwenyezi Mungu.

H-BABA :- ATOA POVU ZITO KWA WASANII WENZAKE

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba miaka ya nyuma na kibao chake cha mpenzi bubu, H.Baba amewachana wasanii wenzake na kusema wanaishi maisha ya uongo.
H. Baba amedai kuwa wasanii wengi sana wanatumia mitandao ya kijamii kufanganya mashabiki kwa pesa za kuazima kwa watu ili tu kuwaaminisha wako vizuri lakini kumbe kiukweli wanaishi maisha magumu sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, H. Baba ametoa povu hilo zito kabisa dhidi ya Wasanii Wenzake ingawa hakutaja majina:

Hii sio mara ya kwanza kwa wasanii kunyoosheana vidole kuwa wanaigiza maisha kwa watu lakini kiuhalisia hali zao ni mbaya.
Wasanii wanaishi maisha ya uongo, anapost picha ana pesa kumbe ameomba kwa jirani apige nazo picha tu lakini ukija kuangalia maisha yake unakuta maisha yake ni magumu sana“.

Monday 21 May 2018

SHAMSA FORD :- SINA BIFU WALA UGOMVI NA HARMONIZE

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kusema hana bifu lolote na staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize hata baada ya kumdhalilisha mume wake .
Wiki chache zilizopita Harmonize alikuwa kwenye vita kali ya Ex wake Jacqueline Wolper na katika ugomvi wao alimtaja mume wa Shamsa Chidi Mapenzi kama mmoja wa mpenzi wa zamani wa staa jambo ambalo lilimkera Shamsa.
Shamsa aliweka wazi kuwa hajafurahishwa na maneno ya Harmonize kumuingiza mume wake Kwenye bifu lake na Wolper na kumdhalilisha wakati anajua wazi kuwa ameoa tayari.
Kwenye mahojiano na FNL ya EATV, Shamsa amesema kuwa licha kutopendezwa na kitendo hicho kwa ujumla hana ugomvi na Harmonize ili maisha mengine yaendelee.
 Mume wangu ni mtu mpole sana, inawezekana hakupendezwa ila alikaa kimya, sisi wanawake tunamunkari ya hali ya juu, halafu unaona huyo kapata wapi huo ujasiri wa kuweka hivyo bila kufikiria hawa watu wengine tayari wana familia zao.
Nilipaniki lakini mwisho wa siku simchukii na sina bifu naye niliongea nilichokuwa najisikia na yameisha na hata tukikutana tunasalimiana vizuri kwa sababu hatuna bifu. Sisi ni vijana tunahitaji kuweka nguvu nyingi sana katika kufanya kazi na sio mabifu”.