Saturday 9 June 2018

T I D:- AIBUKA NA POVU KWA MEDIA ZA BONGO

Msanii TID amesema kuwa utaratibu wa wadau/media kushusha wasanii pale wanapodai maslai yao na kuwapandisha wengine ndio kitu kinaathiri muziki wa Bongo Flava.
Muimbaji huyo ameeleza kuwa kitu hicho ndicho kilitokea kwenye muziki wake na kwa sasa kimemtokea Diamond.

“Na kweli anaweza because he has a media, yaani yeye ndio kama Mungu anajiona but mimi hapana. Nilifanya kosa hilo lakini kosa hilo ndilo limewasanua wasanii wengine, unaona msanii kama Diamond naye amekataa,” amesema.

“So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa tunamleta Diamond tukushushe wewe. At the end Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani,” TID ameiambia Wasafi TV.

TID ameongeza kuwa hajaona kitu kama hicho nchini Kenya kwani bado anamuona Jaguar ni msanii mkubwa, Nonini ni msanii mkubwa anapewa heshima yake hakuna underground yeyote amewekwa pale kumshusha Nonini.

No comments:

Post a Comment