Wednesday 23 May 2018

H-BABA :- ATOA POVU ZITO KWA WASANII WENZAKE

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba miaka ya nyuma na kibao chake cha mpenzi bubu, H.Baba amewachana wasanii wenzake na kusema wanaishi maisha ya uongo.
H. Baba amedai kuwa wasanii wengi sana wanatumia mitandao ya kijamii kufanganya mashabiki kwa pesa za kuazima kwa watu ili tu kuwaaminisha wako vizuri lakini kumbe kiukweli wanaishi maisha magumu sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, H. Baba ametoa povu hilo zito kabisa dhidi ya Wasanii Wenzake ingawa hakutaja majina:

Hii sio mara ya kwanza kwa wasanii kunyoosheana vidole kuwa wanaigiza maisha kwa watu lakini kiuhalisia hali zao ni mbaya.
Wasanii wanaishi maisha ya uongo, anapost picha ana pesa kumbe ameomba kwa jirani apige nazo picha tu lakini ukija kuangalia maisha yake unakuta maisha yake ni magumu sana“.

No comments:

Post a Comment