Monday 28 May 2018

DIAMOND:- SIWEZI KUMUOMBA MSAMAHA ZARI ATA SIKU MOJA

Msanii wa bongo fleva maarufu nchini , Diamond Platinumz kwa mara ya kwanza amefunguka na kuzungumzia swala lake la kuachana na Diamond na kumuomba radhi mwanamama huyo ambapo taarifa za hapo awali ziliwahi kusema kuwa kwa sasa Diamond amekuwa akipiga safari nyingi za Afrika ya Kusini ili kuomba radhi kwa mwanamke huyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari alipoulizwa kuhusu mambo mengi na vijembe vingi ambavyo diamond amekuwa akitupiwa na mwanamama huyo hasa vya hapa karibuni alipokuwa kenya, diamond alisema’ hayo ya kenya bwana tuachane nayo, mimi nadhani yameshapita naomba tuendelee na haya yabsasa itapendeza sana”
Hata hivyo, mwandishi hakuishia hapo ndipo alipoamua kumuuliza moja kwa moja kuhusu yeye kuwa akisafiri kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya kuomba radhi kwa zari huku akienda kwa siri mara kwa mara na diamond alijjibu kuwa safarizake za afrika ya kusini haziusiani na mambo hayo.
Ni muda sasa umepita tangu wawili hao kutengana na kumekuwa na mogogoro mingi kati yao hasa kupitia katika mitandao ya kijamii lakini hii haijamfanya diamond kuacha kuwa na hamu ya watoto wake , mara kwa mara amekuwa akienda kuwaona kama alivyokiri.

ni kweli ninaenda na so mara moja au mara mbili nimekuwa ninaenda,nakwenda kule sio kwa ajili ya kumuomba msamaha , hapana ila ninakwenda kule kwa ajili ya kumuona wanangu tu,haiwezekani niwe ninatuma pesa za matumizi tu alafu ninafka mpaka afrika ya kusini na nisiende kuwaona wanangu.
hao wanaosema kuwa sijui nimekuwa nikimuangukia nadhani yatakuwa ni maoni yao tu wala sio yangu, ni maneno yasiyokuwa na msingi, zari ni mama wa watoto wangu na itabaki kuwa hivyo.

No comments:

Post a Comment