Monday 28 May 2018

ASLAY :- AFUNGUKA KUACHANA NA MAMA WATOTO WAKE

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Aslay Isihaka amekiri kupigana chini na aliyekuwa mpenzi wake na Mama watoto wake Tessy Chocolate.
Siku chache zilizopita kuna tetesi zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wapendanao hao wameachana baada ya Tessy kufuta Tatoo aliyokuwa amechora jina la Aslay mkononi.
Hatimaye Aslay amethibitisha tetesi hizo Kwenye Interview na Bongo 5 ambapo ameweka wazi kuwa yeye na Tessy wamepigana chini na kila mtu anaendelea na maisha yake.
Ingawa Aslay hajaweka wazi sababu ya kuachana lakini inasemekana kuwa alichepuka kwani Tessy alishawahi kudokeza hilo kwa maneno ya mafumbo aliyoposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ni kweli tumezinguana mimi na mama watoto wangu sahivi kidogo kila mtu anaangalia maisha yake ila mimi na yule ni ndugu tumezaa tuna mtoto wetu tunashukuru mtoto wetu anaendelea vizuri hilo ndo la maana”.

No comments:

Post a Comment