Showing posts with label Fulsa/Maujanja. Show all posts
Showing posts with label Fulsa/Maujanja. Show all posts

Tuesday, 10 December 2019

JINSI YA KUTENGENEZA SAMBUSA ZA NYAMA


                                                                      Nyama steki kilo 1 ( mi nina mashine ya kusagia kama huna nunua ya kusaga)
.
.Vitunguu maji 2
.
 Majani ya Giligiliani vifungu 2 .
.Garam masala kijiko 1 cha chai
.
.Chumvi kijiko 1 cha chai
.
.Pilipili manga kikijo 1 cha chakula
.
.Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai
.
.Tangawizi ya Unga kijiko 1 cha chai
.
.Karoti 2 kubwa
.
.Pilipili hoho 2
.
.Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai
.
.Manda
.
.Butter kijiko kimoja cha chakula
.
.
.Maelekezo
.
.Bandika nyama weka chumvi, mpaka iive iwe laini. .
.Hamisha supu pembeni ibaki nyama tu.
.
.Chukua mashine ya kusagia nyama, weka giligilia kwenye nyama, anza kusaga nyama na giligiliani pamoja, funika weka pembeni.
.
.Kata kata vitunguu maji, muundo wa box size ndogo sana, kata karoti na pilipili hoho. Weka pembeni.
.
.Chukua frying pan pana, weka butter au mafuta ya kawaida. Ikianza kuchemka weka vitunguu maji, karoti na pilipili hoho, koroga visiive.
.
.Weka kitunguu saumu kilichosagwa, weka pilipili manga na tangawizi koroga vizuri.
.
.Weka nyama, koroga vizuri ili ichanganyikane na viungo vingine, weka garam masala .
.
.koroga dakika 2, epua. Usiifunike
.
.Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
.
.Chukua manda, kata kwa umbo la pembetatu. Kisha weka nyama kiasi, anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga.
.
.Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
.
.Bandika mafuta yakipata moto anza kupika,mpaka uone sambusa zimegeuka rangi na kua kahawia. .
.Epua anza kujiramba.


JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI NZITO YA KUOSHEA VYOMBO: .


                                                                           
.MAHITAJI:
.
.Sulphonic acid lita moja
.
.soda ash robo kilo
.
.Sless au ungalol  lita 1
.
Glyceline vijiko vitano vya chakula
.
.Rangi kijiko kimoja
.
.Chumvi gram 750
.
.Tigma ya 3000
.
.pafyum laini ya matunda au harufu uipendayo
.
.CDE mls 2000
.
.Maji Safi lita 40.
.
⚪KUTENGENEZA
 Chukua Maji Lita 40 gawa Mara mbili ili upate Lita 20. Kisha Lita 20 Moja tia tigna yote koroga hadi kupata uji mzito kisha well kando.weka Sulphonic acid kwenye Chombo kisha to soda ash kisha koroga vyema Hadi kupata kitu Kama ugali HAKIKISHA unakoroga vyema kwa muda wa dakika 20 bila kupumzika .
.
.Kisha ongeza Sless koroga vyema kwa dakika 10 kisha tia Maji Lita 20 ambayo hayana Tigna kisha koroga hadi ule ugali uishe wote (tumia fagio la chelewa Safi kukorogea ili kurahisisha)
.
.Baada ya hapo tia Yale Maji yenye Tigna, koroga vyema kisha ongeza rangi na glycerine, CDE, endelea kukoroga Hadi iishe kisha mwisho tia Pafyumu na ukoroge kwa dakika 5 na acha sabuni iive,
.
.Ifunike na uiache kwa masaa 24 na zaidi ndio ufungashe katika vifungashio, peleka sokoni
.
. Vifaa vinapatikana katika maduka ya Ujasiriamali .
.

JINSI YA KUANDAA DAGAA WA KUKAANGA NA UKAUZA BILA KUHARIBIKA KWA MWEZI 3


                                                                               .DAGAA WA KUKAANGA WATAMU:
.
.Mahitaji:
.
.🔸Dagaa wabichi 1/2 kilo .
.🔸Chumvi na pilipili manga kiasi
.
.🔸Unga wa ngano kijiko kimoja Cha chai
.
.🔸soy source vijiko viwili vya chai
.
.🔸Tangawizi ya unga kijiko 1 cha cha chai
.
.🔸Vipande vya ndimu .
.🔸Pilipili nyekundu ya unga kijiko 1 cha chai au kiasi chako (ukipenda)
.
.🔸Kitunguu swaumu Cha unga nusu kijiko Cha chai
.
.NAMNA YA KUTAYARISHA:-
.
.1. Safisha vizuri dagaa wako kisha wacha wachuje maji katika chujio.
.
.2. Wakishachuja maji watie viungo vyote changanya vizuri waenee kisha waache dk 15-30 waingie vizuri viungo.
.
.3. Tia Mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi, yakipata moto, watie daga wako katika unga waenee kisha tia katika mafuta moto na kaanga hadi wapate rangi nzuri
.
.4. Epua na wacha wachuje mafuta katika chujio au wire. Utarudia kumaliza dagaa wote.
.
.5. Dagaa tayari kwa kula kwa vipande vya ndimu pembeni na ugali au upendavyo.
.
.

JINSI YA KUTENGENEZA POPCORN ZA SUKARI BILA MASHINE


P
                                                                                ________________________________________
Weekend snack  Mahitaji:

Mahindi ya popcorn kiasi
Mafuta
Sukari
Iriki robo kijiko

Jinsi ya kutengeneza:

Chukua sufuria weka jikoni tia mafuta yakipata moto kidogo tuu tia mahindi ya popcorn koroga yale mahindi mpaka yakianza kupasuka funika sufuria na yageuze geuze kwa pepeta sufuria mpaka yote yapasuke yakishapasuka toa weka pembeni chukua sufuria lingine tia sukari kiasi unachopenda na iriki  na ibandike jikoni mpaka sukari ikianza kuyayuka tia popcorn zako huku ukiwa unakoroga polepole zote ziingie sukari vizuri baada ya hapo ipua weka ipoe ikisha poa enjoy popcorn zako zitakua tayari kwa kuliwa, au funga kwa biashara