Tuesday 10 December 2019

JINSI YA KUANDAA DAGAA WA KUKAANGA NA UKAUZA BILA KUHARIBIKA KWA MWEZI 3


                                                                               .DAGAA WA KUKAANGA WATAMU:
.
.Mahitaji:
.
.🔸Dagaa wabichi 1/2 kilo .
.🔸Chumvi na pilipili manga kiasi
.
.🔸Unga wa ngano kijiko kimoja Cha chai
.
.🔸soy source vijiko viwili vya chai
.
.🔸Tangawizi ya unga kijiko 1 cha cha chai
.
.🔸Vipande vya ndimu .
.🔸Pilipili nyekundu ya unga kijiko 1 cha chai au kiasi chako (ukipenda)
.
.🔸Kitunguu swaumu Cha unga nusu kijiko Cha chai
.
.NAMNA YA KUTAYARISHA:-
.
.1. Safisha vizuri dagaa wako kisha wacha wachuje maji katika chujio.
.
.2. Wakishachuja maji watie viungo vyote changanya vizuri waenee kisha waache dk 15-30 waingie vizuri viungo.
.
.3. Tia Mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi, yakipata moto, watie daga wako katika unga waenee kisha tia katika mafuta moto na kaanga hadi wapate rangi nzuri
.
.4. Epua na wacha wachuje mafuta katika chujio au wire. Utarudia kumaliza dagaa wote.
.
.5. Dagaa tayari kwa kula kwa vipande vya ndimu pembeni na ugali au upendavyo.
.
.

No comments:

Post a Comment