Tuesday 10 December 2019

JINSI YA KUTENGENEZA SAMBUSA ZA NYAMA


                                                                      Nyama steki kilo 1 ( mi nina mashine ya kusagia kama huna nunua ya kusaga)
.
.Vitunguu maji 2
.
 Majani ya Giligiliani vifungu 2 .
.Garam masala kijiko 1 cha chai
.
.Chumvi kijiko 1 cha chai
.
.Pilipili manga kikijo 1 cha chakula
.
.Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai
.
.Tangawizi ya Unga kijiko 1 cha chai
.
.Karoti 2 kubwa
.
.Pilipili hoho 2
.
.Unga wa ngano vijiko 4 vya chakula au ute wa yai
.
.Manda
.
.Butter kijiko kimoja cha chakula
.
.
.Maelekezo
.
.Bandika nyama weka chumvi, mpaka iive iwe laini. .
.Hamisha supu pembeni ibaki nyama tu.
.
.Chukua mashine ya kusagia nyama, weka giligilia kwenye nyama, anza kusaga nyama na giligiliani pamoja, funika weka pembeni.
.
.Kata kata vitunguu maji, muundo wa box size ndogo sana, kata karoti na pilipili hoho. Weka pembeni.
.
.Chukua frying pan pana, weka butter au mafuta ya kawaida. Ikianza kuchemka weka vitunguu maji, karoti na pilipili hoho, koroga visiive.
.
.Weka kitunguu saumu kilichosagwa, weka pilipili manga na tangawizi koroga vizuri.
.
.Weka nyama, koroga vizuri ili ichanganyikane na viungo vingine, weka garam masala .
.
.koroga dakika 2, epua. Usiifunike
.
.Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
.
.Chukua manda, kata kwa umbo la pembetatu. Kisha weka nyama kiasi, anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga.
.
.Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
.
.Bandika mafuta yakipata moto anza kupika,mpaka uone sambusa zimegeuka rangi na kua kahawia. .
.Epua anza kujiramba.


No comments:

Post a Comment