Msanii wa filamu za Bongo, Wastara Juma, tayari ameshawasili nchini India na kuanza rasmi matibabu ya mguu wake katika Hospitali ya Saifee nchini humo.
Wastara ambaye alichangiwa fedha na Watanzania mbalimbali walioguswa na hali yake pamoja na Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli, aliondoka nchini juzi Jumapili, Feb. 4, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Msanii huyo maarufu amekuwa akisumbuliwa na mguu wake huo ambao ulipelekea kufanyiwa upasuaji na kupewa mguu wa bandia licha ya hali yake kubadiilika hivi karibuni na kudai kuwa amekuwa akipata maumivu makali ambapo baada ya kupata matibabu ya awalialishauriwa kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.
Akizungumza na mtandao wa #Ragbu One Wastara amewashukuru Watanzania kwa michango yao kufanikisha matibabu yake.
“Nawashukuru Watanzania wote waliojitoa kunichangia ili niweze kupata matibabu, Namshukuru Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth, peke yangu nisingeweza. Tulisafiri salama, tunamshukuru Mungu tumefika salama, kwa sasa nimeanza matibabu katika Hospitali ya Saifee hapa India.
“Kiafya nashukuru kwa kweli, najiskia vizuri kiasi japo bado mapema kuzungumzia maendeleo ya afya yangu kwa ujulma, lakini nawaombeni muendelee kuniombea kwa Mungu ili nipone, nirudi nyumbani salama,” amesema Wastara
No comments:
Post a Comment