Tuesday, 6 February 2018

MOHAMMED SARAHA:" Awapiga bao Manchester United AND Chelsea

Kwa sasa zungumzia mastriker hatari zaidi nchini Uingereza na duniani huwezi kuacha jina la mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah ambaye msimu huu anaonekana kutozuilika.Hadi sasa Salah ana mabao 21 katika ligi ya EPL lakini uwezo wake wa kufunga mabao kwa juhudi binafsi umemfanya kuonekana striker bora zaidi katika ligi ya EPL lakini Salah ana jambo kubwa lingine.Usilolijua ni kwamba hadi sasa katika msimu huu wa EPL Mo Salah ana mabao mengi dhidi ya timu sita za juu katika ligi hiyo na idadi yake ya magoli dhidi ya timu hizo ni kubwa kuliko mabao ya Manchester United na Chelsea. Salah amezifunga timu za 6 bora jumla ya mabao 7 hadi hivi sasa hiku Chelsea wenyewe wakiwa wamezifunga timu za 6 bora jumla ya mabao 6 msimu huu  huku Manchester United wakiwa wamefunga mabao 5.Bao la 20 la Mo Salah limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufika idadi kubwa ya mabao katika mechi chache (25) japo mwaka 1909 Ronald Orr  alishawahi kufikisha idadi kama hiyo ya mabao katika mechi chache zaidi (23).

No comments:

Post a Comment