Tuesday, 6 February 2018

ROONEY:" Afunguka ukweli kuhusu Sanchez, Pogba, Makhtaryan na Man city

Kabka ya mechi ya jana kati ya Watford na Chelsea mchezaji wa zamani wa Manchester United WayneRooney aligeuka mchambuzi katika kituo maarufu cha michezo nchini UK cha Sky Sports.Moja kati ya mambo makubwa ambayo Wayne Rooney aliyazungumzia ni kuhusu wachezaji watatu ambao wamekuwa katika vichwa vya habari vingi katika siku za usoni (Paul Pogba, Henrikh Mkhitaryan na Alexis Sanchez).Kwanza kuhusu Henrikh Mkhitaryan na Alexis Sanchez, kuhusu Mkhitaryan, Rooney anaamini mchezaji huyo kwa sasa yuko katika sehemu sahihi zaidi tofauti na alipokuwa katika klabu ya Manchester United.Wayne Rooney ambaye alikuwa pamoja na Mkhitaryan katika kikosi cha United na anasema Mualmernia huyo ana kipaji kikubwa sana lakini alishindwa kuwa bora kutokana na kukosa uhuru aliokua akiupata United.Kuhusu Sanchez, Rooney anaamini bila shaka kwamba Sanchez ni mtu sahihi kabisa kwa Manchester United na hata ukimuangalia tu jinsi ameingia katika klabu hiyo anaonesha amekuja kikazi zaidi.Rooney anasema kati ya vitu Romelu Lukaku alivyokuwa anavikosa ndani ya Manchester United ni wachezaji ambao wanamsukuma mbele ili afunge na ujio wa Sancheza unaweza kuwa tiba la suala hilo.Paul Pogba, Wayne anasema kama Pogba akipunguziwa majukumu anaweza kuwa bora zaidi kwani Pogba ni mzuri zaidi akicheza box to box midfilder na kwa uwepo wa Matic inaweza kumuimarisha siku hadi siku.Kuhusu Manchester City Rooney ameweka wazi kwamba kuwakamata haiwezekani na akasisitiza kwamba kwa jinsi wanavyocheza soka hata msimu ujao pia inawezekana wasikamatike

No comments:

Post a Comment