Wednesday, 7 February 2018

Wanaume wa kazi Waweka Rekodi zao Ulaya


Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Alexies Sanchez.
LIGI Kuu England iliende­lea wikiendi iliyopita huku ikiwa na mambo mengi mapya ambayo mashabiki wa soka walikuwa wakiyasubiri kwa hamu kubwa.
Mashabiki walishuhudia wache­zaji wengi wapya wakizitumikia timu zao na kuonyesha kiwango cha hali ya juu sana huku wengine wakianza kwa kuchemka.

Hii ndiyo imekuwa ligi ambayo in­afuatiliwa na mashabiki wengi sana wa soka duniani kote na hii imewa­saidia wachezaji wengi sana kupenda kwenda kutumika kwenye ligi hiyo.
Lakini chini ni rekodi zilizowekwa na wachezaji kadhaa timu na na mashabiki wa Ligi Kuu England.
Mshambuliaji wa Tottenham Hortspur, Harry Kane.
KANE 100
Mshambuliaji wa Tottenham Hortspur, Harry Kane wikiendi iliyopita aliifungia timu yake bao moja kwenye sare ya mabao 2-2 na dhidi ya Liverpool na kufikisha mabao 100, kwenye timu hiyo baada ya kuichezea michezo 141 kwenye Ligi Kuu Eng­land.
Kiungo mpya wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan.
WANYAMA 8
Kiungo wa Tottenham, Victor Wanyama timu yake imepata ushindi mara nane huku nyuma akiwa yeye amefunga bao.

DELE 3
Kiungo wa Spurs, Dele Alli amepewa kadi tatu za njano msimu huu kutoka­na na kumdanganya mwamuzi, hakuna mchezaji aliyepewa kadi nyingi hivyo hadi sasa.

SALAH 20
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amefanikiwa kufunga mabao 20 kwenye michezo 25 tu ya Ligi Kuu England ambayo ameichezea Liverpool msimu huu.
Huyu ndiye mchezaji aliyeichezea Liver­pool michezo michache na kufunga ma­bao mengi.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp
KLOPP 12
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp hajafun­gwa kwenye michezo 12 ya Ligi Kuu England ambayo amekutana na timu zilizopo kwenye sita bora kwenye Ligi Kuu England. (Ameshin­da 6, ametoka sare 6).

PALACE 6
Timu ya Crystal Palace imepewa penalti sita kwenye Ligi Kuu England msimu huu, tano kati ya hizo wamepewa kwenye Uwanja wa Selhurst Park. Ni Everton tu ndiyo wamepewa penalti nyingi kuliko wenyewe, wamepewa saba.

DIAME 5
Mabaoa matano yote aliyofunga Mohamed DiamĆ© wa New­castle United kwenye Ligi Kuu England amefunga kutoka nje ya uwanja wao wa nyumbani St James.

MKHITARYAN 3
Kiungo mpya wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan amekuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kutoa pasi tatu za mabao kwenye mchezo mmo­ja wa Ligi Kuu England tangu Santi Cazorla alipopiga nne, mwaka 2013.

RAMSEY 20
Kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey ni mchezaji wa 20 kufunga hat trick kwenye timu hiyo, hii ndiyo timu iliyofunga hat trick, nyingi kuliko nyingine zote.

CECH 6
Kipa wa Arsenal Petr Cech ametolewa uwanjani mara sita kwenye michezo ya Ligi Kuu England, mara tatu kati ya hizo ametolewa kwenye mchezo dhidi ya Everton.

ARSENAL 4
Arsenal ni timu ya pili kwenye Ligi Kuu England kufunga mabao manne kwenye dakika 45 za kwanza, timu ya kwanza kufunya hivyo ni ni Man United ilifunga No­vemba 1997.

AUBAMEYANG 8
Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Pierre-Em­erick Aubameyang amekuwa mchezaji wa nane kuanza mchezo wake wa kwanza kwenye timu hiyo na kufunga bao.

RAMSEY 100
Kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey amehusika kwenye mabao 100 kwenye timu yake ya Arsenal kwenye michuano yote. ( Ame­funga mabao 52, ametoa pasi 48).

SANCHEZ 7
Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Alexies Sanchez, alichezewa faulo mara saba kwenye mchezo dhidi ya Huddersfield, ndiye mchezaji aliyechezewa rafu nyingi zaidi kwenye mchezo mmoja kwenye ligi.

MAN CITY 1
Mchezaji wa Man City dhidi ya Burnley ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 wikiendi iliyopita ndiyo mchezo wa kwanza timu hiyo inashindwa kushinda baada ya kuanza ku­funga bao.

OZIL 2013
Baada ya kuanza kucheza mchezo wa kwanza kwenye Ligi Kuu Eng­land mwaka 2013, kiungo wa Arse­nal, Mesut Ozil ametengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga kufunga kuliko wachezaji wengine wote.
FIRIMINO 10
Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino amefanikiwa kuhusika kwenye mabao kumi kila anapocheza na timu ambayo imepanda daraja. (Amefunga mabao nane, na kutoa pasi mbili).

GIROUD 17
Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud amefanikiwa kufun­ga mabao 17 akiwa anatokea kwenye benchi ni Jermain Defoe tu amefunga mabao mengi kuliko Mfaransa huyo amefunga ma­bao 23.

No comments:

Post a Comment