UCHUNGUZI wa vinasaba (DNA) uliofanywa karibuni umeonyesha kwamba Mwingereza aliyeishi miaka ipatayo 10,000 alikuwa na ngozi nyeusi, macho ya bluu na nywele nyeusi, ndefu zenye kujipindapinda.
Utafiti huo ulitokana na mabaki ya fuvu na mifupa kamili ya binadamu aliyekufa miaka 10,000 iliyopita aitwaye Cheddar Man ambavyo vilichimbuliwa eneo la Cheddar Gorge, Somerset, Uingereza, mwaka 1903 na ambapo mabaki hayo yanasemekana kuhusiana kinasaba na mtu mmoja kati ya kumi nchini Uingereza leo.
Vipimo vilivyochukuliwa vinaonyesha kwamba asilimia 76 ya mtu huyo wa Cheddar, alikuwa mtu mweusi ambapo inaonyesha pia kwamba wakazi wa visiwa vya Uingereza, walikuja kupata ngozi nyeupe baadaye kutokana na mazingira yaliyokuwepo.
Wakati wa Cheddar Man anafariki, idadi ya watu nchini Uingereza ilikuwa ni 12,000 ambapo vinasaba vya mtu huyo leo hii vimepatiana katika nchi zingine za Ulaya huko Hispania, Hungary na Luxembourg.
Wanasayansi wanasema pia kwamba mababu wa Cheddar Man waliingia Uingereza kupitia Mashariki ya Kati baada ya kuondoka barani Afrika.
WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI
No comments:
Post a Comment