MIMI Mars ni miongoni mwa wanadada wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva. Jina lake alilopewa na wazazi wake ni Marianne Mdee na ni mdogo wa damu wa mwanamuziki Vanessa Mdee ‘Vee Money’.
Mbali na kuwa mwanamuziki, Mimi Mars ambaye hana muda mrefu kwenye gemu lakini akiwa na nyimbo kali zikiwemo Nadata, Shuga na wimbo mpya wa Sitamani, pia ni mtangazaji wa televisheni.
Katika makala haya Mimi Mars amefunguka mambo mengi kuhusu muziki wake pamoja na maisha binafsi.
One: Ujio wako mpya mapokezi yake yamekuwaje?
Mimi Mars: Ukweli ni kwamba mapokezi yamekuwa mazuri, wimbo umefanya vizuri ndani na nje ya Bongo na hata idadi ya watu wanaonisapoti wameongezeka kiukweli.
One: Kwa uonavyo wewe, nani ni mshindani wako kwenye muziki Bongo?
Mimi Mars: Kiukweli sina mshindani, kila mwanamuziki anafanya muziki kwa namna yake mwenyewe, kwa hiyo mshindani wangu naweza kusema ni mimi mwenyewe. Nashindana kila siku ili kuleta mvuto zaidi kwenye kazi zangu.
One: Mwanamuziki gani wa kike anakuvutia na ambaye unapenda kufanya naye kazi ndani na nje ya Bongo?
Mimi Mars: Kiukweli wanamuziki wanaonivutia ni wengi ndani na nje ya Bongo. Lakini sana ningependa kufanya kazi na wanamuziki wa nje ya nchi wakiwemo Yemi Alade, Seyi Shay, Tiwa Savage, Niniola, Fena, Victoria Kimani, kiukweli listi ipo ndefu sana.
One: Tumeona Vee Money ametoka na albamu, wewe pia ni miongoni mwa timu yake, mipango ya kutoa albumu kwako ipo vipi?
Mimi Mars: Mpango wa kutoa albumu labda mwakani, lakini kwa sasa ninataka mashabiki wangu waifahamu sauti yangu na nguvu yangu ya muziki ili nitakapotoa albumu waweze kuifurahia zaidi.
One: Mpaka sasa tangu uanze muziki ni mafanikio gani makubwa umeweza kuvuna?
Mimi Mars: Mafanikio ni makubwa sana na yanazidi kumiminika. Nimevuna mashabiki wengi, nimefanya matamasha makubwa mpaka nje ya nchi, kule Kenya. Lakini pia nimekuwa kwenye nomination za tuzo za Ami Afrika na ninaomba mashabiki wa muziki wanipigie kura ili tulete tuzo nyumbani kwenye kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki.
One: Kazi zako zinasimamiwa na nani?
Mimi Mars: Ninasimamiwa na menejimenti ya Mdee Music pamoja na watu mbalimbali ambao wanahakikisha kazi zangu zinakwenda vizuri na katika mpangilio mzuri.
One: Una kolabo ya nje yoyote ambayo umekwisha kufanya au unatarajia kufanya hivi karibuni?
Mimi Mars: Kolabo zipo nyingi na mashabiki watakwenda kuzisikia hivi karibuni. Maana mwaka huu ndiyo mwaka wa kila kitu kwangu kimuziki, yaani kufika mbali zaidi.
One: Katika masuala binafsi, kipi amb-acho huki-pendi kwenye maisha yako?
Mimi Mars: Kiukweli sipendi uongo na unafiki. Unajua watu wa namna hii wanaweza hata kukuua, kwa hiyo hivyo ni vitu ambavyo sivipendi kabisa.
One: Una mpenzi au mume na anaitwa nani?
Mimi Mars: Sina mpenzi, sina mume na akitokea huko siku za usoni bila shaka kila mmoja atafahamu.
One: Unamzungumziaje Jux kama shemeji yako, kwako binafsi anapendeza kuwa na Vee Money na unawaona wapi katika uhusiano wao siku za usoni?
Mimi Mars: Jux ni mtu poa kusema kweli. Naweza kusema ni zaidi ya shemeji kwangu. Anajali, ana upendo wa dhati. Ana upendo na heshima. Na ninashukuru anavyompenda Vanessa. Ninaona anamfanya pia kuwa mtu bora katika kazi na hata maisha yao ya kawaida na ninawaona mbali.
Kama mwanafamilia ninafahamu wana mipango yao mikubwa, wakiamua ‘kushare’ na mashabiki watawaeleza, wasipoamua pia kama wanafamilia bado tunawaona mbali.
O: Mengine ambayo ungependa kuzungumzia kuhusu muziki wako?
Mimi Mars: Ninashukuru kwa kila mtu anayenisapoti. Pia kwa ambao hawajasikiliza muziki wangu ningependa wasikilize, bila shaka wataipata sababu ya kunisikiliza. Sitawaangusha kama ambavyo nimekuwa nikisema mara zote. Asa-nte-ni
No comments:
Post a Comment