Wednesday, 7 February 2018

CHADEMA "" Prof-Jay... Azuiliwa kumuona "Sugu"

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa kimedai kuwa mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof. Jay na mkewe wamezuiliwa kuwanona Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga katika Gereza la Ruanda ambako wamewekwa mahabusu.

Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ akiwa ameambatana na Mkewe Grace Haule amefika Mbeya jana na leo tarehe 07 Februari 2018 ameenda katika Gereza la Ruanda mkoani humo kwa ajili ya kuwaona Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga ambapo amekataliwa kuwaona na uongozi wa Gereza hilo

Viongozi hao Sugu na Masonga wanaoshikiliwa kwa kunyimwa dhamana kesho Alhamisi tarehe 08 Februari 2018 watafikishwa mahakamani kwa ajili ya muendelezo wa kesi yao ambayo wanatuhumiwa kwa kutoa maneno ya fedheha.
Habari – CHADEMA
Kanda ya Nyasa
O7 Februari 2018.
Chadema Kanda ya Nyasa

No comments:

Post a Comment