Thursday, 8 February 2018

Viongozi wawili wa IS wakamatwa

Taarifa zinasema kuwa raia wawili wa Uingereza wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislam cha IS wanashikiliwa na kundi la wapigaji wa Kikurd.
Wakurd wasisitiza kujitenga na Iraq
Majeshi ya Iraq, yasonga mbele Kirkuk
Wanamgambo 250 wa IS waliondoka Raqqa
Alexanda Kotey mwenye umri wa miaka 34 na mwenzake El Shafee Elsheikh mwenye miaka 29 ni miongoni mwa vijana wawili waliokuwa wanasakwa kati ya wenzao ambao walikwisha kukamatwa.
Kundi hili la vijana wanne kutoka raia wa Uingereza ndani ya kundi la IS walikuwa ni kundi hatari linalofahamika kama Beatles hiyo ikiwa ni kutokana na lafudhi yao wanapozungumza.
Maofisa wa Marekani wamesema kuwa kundi hilo lililokuwa likihusika na utoaji mateso pamoja na kuua ndani ya IS linadaiwa kuwachinja Zaidi ya watu 27 mateka kutoka nchi za kimagharibi na kutoa mateso makali kwa wengine wengi tu.
Beatles ni akina nani hasa?
Hawa ni kundi hatari kwaajili ya mauaji na mateso,ambalo lilikuwa linajumuisha watu kama Mohammed Emwazi almaarufu kama Jihadi John ambaye alikuwa akionekana katika picha za video akiwa anachinja watu.Aliuawa katika mashambulizi ya anga mwaka 2015 katika mji wa Raqqa ngome ya zamani ya IS.
Lakini wapo pia Aine Davis ambaye naye alikuwa akitokea Uingereza,alihukumiwa baada ya kubainika kuwa alikuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa kundi la Islamic State na alifungwa mwaka jana huko Uturuki.Wengine wanaounda kundi hili la Beatles ni Alexanda Kotey ambaye naye anatoka London magharibi,yeye alikuwa katika kitengo cha utesaji,kwa mjibu wa Marekani na alikuwa mtu anaye toa usajili kwa wanaojiunga na IS.
El Shafee Elsheikh huyu yeye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda genge hili,hawa ndiyo Beatles.

     

No comments:

Post a Comment