ANAFAHAMIKA zaidi kwa jina la Tunda, na ukimdadisi sana ataishia kukwambia kwamba jina lake halisi anaitwa Tunda Sebastian, namzungumzia huyu msichana ambaye kila kukicha haishiwi na vituko mjini.
Huwa sijui ni kwa nini hapendi uhalisia wake ujulikane, likiwemo jina lake halisi. Licha ya kufahamika na wengi kama Tunda Sebastian, jina lake halisi anaitwa Anna Patric Kimario, wanaomjua wanasema amekulia mkoani Morogoro ingawa kuna wakati pia aliishi Moshi na Kijichi hapa Dar es Salaam, hiyo ilikuwa ni kabla hajaanza maisha yake ya kimjinimjini.
Tunda anajinasibu kwamba kazi inayomuweka mjini ni ‘u-video queen’. Kwa wasioelewa maana yake, hawa ni wale wasichana wanaoonekana kwenye video za wasanii, hasa hawa wa Bongo Fleva.
Ukizungumzia kazi yake, japokuwa wengi wanaweza kuwa hawajui, lakini Tunda amefanya kazi kadhaa, japo siyo kivile lakini huwezi kumuondoa kwenye orodha ya wasichana ambao ukiwaweka kwenye video yako kama wewe ni msanii, basi hawezi kukuangusha.
Kazi yake mpya kabisa, ni kwenye video ya barnaba aliyomshirikisha Aslay, iitwayo Ngoma ambapo Tunda amecheza kama Maria, binti aliyekulia kijijini ambaye ameenda kuposwa na sasa anapewa nasaha za namna ya kuishi kwenye ndoa. Hebu itazame tena utakubaliana nami kama Tunda anacho kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yake.
Ukiacha kazi hii mpya, zipo nyingine za kitambo kidogo ambazo Tunda amefanya kazi nzuri! Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! Tazama video kama Why Me ya Amini na Barnaba, video ya wimbo wa Matonya aliyomshirikisha Christian Bella uitwao Agwelina, mtazame kwenye video ya Raha ya TID!
Mcheki kwenye Sina Makosa ya Timbulo na video nyingine kadhaa alizouza nyago! Ninachotaka kukuonesha hapa ni kwamba japokuwa wengi hawamuelewi msichana huyu kama anajishughulisha na nini hasa, anacho kipaji, anayo kazi ambayo inamuingizia kipato na kama akiamua kuwekeza nguvu huko, anaweza kuishi maisha ya juu pengine kuliko haya anayofosi sasa.
U-video queen au wengine wanaita video vixen, ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na upo ushahidi mkubwa wa watu waliofanikiwa sana kwa kazi hiyo, mfano mzuri ni kama mwanadada Tokyo anayeonekana kwenye video ya Kendrick lamar iitwayo backstreet Freestyle, au mwanadada mwingine Alisha Jenay ambaye ameng’ara kwenye video kibao mbele, hasa za hip Hop na kubwa kuliko ni mwanadada Esther Baxter, kama humjui itazame video ya The New Workout Plan ya Kanye West.
Baxter anatajwa kuwa ndiye video vixen mwenye mafanikio zaidi kwenye tasnia hiyo, hatua ambayo hata Tunda leo akiamua, anaweza kuifikia.
Unaweza kujiuliza, kwa nini namzungumzia Tunda? Huyu ‘mtoto’, licha ya umri wake mdogo usiozidi miaka 24, amesheheni matukio, tena mazitomazito, mengi yakihusisha skendo za ngono! Tena na wanaume ambao wamemzidi sana umri!
Fuatilia akaunti yake ya Instagram, utagundua kwamba Tunda anapenda sana maisha ya juu, kutwa kucha kuzurura kwenye mahoteli makubwa, kazi yake kubwa ni kula bata! Tena kwenye viwanja vyenye hadhi ya juu!
Unaweza kujiuliza, ni pesa mbuzi anazolipwa na hawa wasanii wanaomtumia kwenye video zao ndizo zinazompa jeuri ya kutamba kiasi hiki? La hasha! Yapo madai mazito kwamba mwanadada huyu ameamua kutafuta mafanikio kwa njia ya mkato, anautumia mwili wake kama kitega uchumi!
Ni madai mazito kuliko umri wake! Na kwa bahati mbaya au nzuri, yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele wa kuthibitisha hilo kwa vitendo!
Tazama picha anazoposti, tazama video zinazotembea mitandaoni, zikimuonesha akifanya matendo yasiyofaa kufanywa hadharani, kwa binti kama yeye, tena na wanaume ambao wengine wangeweza kumzaa! Rejea video yake akidendeka na mtoto wa marehemu Kingunge Ngombale Mwiru aitwaye Kinjekitile au Kinje!
Orodha ya wanaume wanaotajwa kubanjuka naye ni ndefu! Yupo Diamond Platnumz na wengine wengi, wakubwa kwa wadogo, mastaa kwa wasio mastaa! Achana na skendo hiyo, amewahi pia kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, sitaki sana kuzungumzia huko, yawezekana zilikuwa ni tuhuma tu!
Ninachotaka kukwambia Tunda, achana na njia za mkato, acha kutumia vibaya uzuri Mungu aliokujaalia, hebu jiulize, miaka kumi ijayo utakuwa wapi? Haya unayoyafanya leo, ya kujiona kama bado wewe ni mtoto mdogo, yatakupeleka wapi?
Acha michezo ya hatari kwenye zama hizi zilizojaa magonjwa yakiwemo Ukimwi, tulia ufanye kazi! Wanaume watakutumia na kukuacha kwenye mataa, akili kumkichwa maana muda haukusubiri! Take care
No comments:
Post a Comment