Thursday 15 February 2018

TIMBULO & ABDU KIBA """"waingia Vitani

TIMBULO NA ABDU KIBA WAINGIA VITANI

Msanii wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba amejikuta kwenye mvurugano na msanii mwenzake Timbulo baada ya kituhumiana kuibina mashairi ya nyimbo.

Wasanii hawa wawili waliingia katika mgogoro mkubwa sana Timbulo na Abdu Kiba baada ya wote wawili kujikuta wanaimba mashairi yanayo fanana huku Timbulo akimtupia lawama na kumuuliza kwa nini atumie mashairi yake.

Kizaazaa hiki kilianza baada ya habari kusambaa kuwa kuna rekodi ambayo imefanywa na Timbulo na kumshirikisha msanii mwingine anayeitwa Promise ambayo inafanana kabisa mashairi na nyimbo mpya ya Abdu Kiba inayoitwa jeraha.

Baada ya hapo kilichotokea ni kila mtu anamrushia mwenzake maneno na kumlaumu kwa kumuibia mashairi. Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Timbulo amefunguka na kusema anamlaumu Abdu Kiba kwa kumuibia mashairi yake:

No comments:

Post a Comment