MWANADADA ambaye anakimbiza kwenye tasnia ya Muziki wa Hip Hop Bongo, Claudia Lubalo ‘Chemical’, ametokwa povu baada ya kuambiwa kwamba ameanza kufulia ndiyo maana hasikiki tena kwenye media kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kabla ya wanadada wengine kuibuka.
Akipiga stori na ragbuone, Chemical alisema maneno hayo yameibuka kwenye mitandao pengine kutokana na mashabiki wake kuona ‘ame-base’ kwenye muziki wa Singeli lakini si kweli kama amefulia bali anajaribu kufanya kila analoweza kwenye muziki ili kuonesha utofauti kati yake na wanamuziki wengine.
“Siwezi kufulia hata siku moja, Chemical ni kiwanda ambacho kinajitosheleza kwa uzalishaji wa muziki, kwa hiyo watu wanaodhani kwamba nimefulia wanakosea sana na kiukweli wategemee kuona mengi kutoka kwangu kwa mwaka huu,” alimaliza Chemical
No comments:
Post a Comment