Thursday 15 February 2018

ZIDANE ni kitu gani kitanibakisha Real Madrid!!

Zinedine Zidane ni miongoni mwa wale ambao hawawezi kuelezea sababu ya matokeo mabaya ya timu hiyo, na inaonekana kana kwamba ameshindwa na mawazo ya kubadilisha mambo katika klabu hiyo.
Iwapo Real Madrid watabanduliwa katika michuano ya klabu bingwa na Paris St Germain, itakuwa vigumu kwa yeye kusalia hadi msimu ujao. Je meneja ambaye amefanikiwa kushinda kombe la vilabu bingwa Ulaya katika misimu miwili ya ukufunzi wake mbali na taji la La Liga msimu uliopita anaweza kukabiliwa na shoka?.
Siku ya Jumatano 16 Agosti: Real Madrid 2-0 Barcelona
Baada ya msimu mpya kuanza kulikuwa hakuna ishara ya kuwepo kwa tatizo lolote katika klabu hiyo huku Real Madrid ikiicharaza Barcelona 5-1 kwa jumla katika kombe la Supercup baada ya kuishinda Man United na kubeba kombe la Uefa Cup.
Beki wa Barcelona Gerrard Pique: Lazima tukubali kwamba Madrid ni wazuri kutuliko. Katika kipindi cha miaka tisa nilichohudumu hapa nahisi ni wakali kutuliko.
Siku ya Jumamosi , 9 Septemba: Real Madrid 1-1 Levante
Ishara za kwanza za kutia wasiwasi zilianza kuonekana katika mechi zao mbili za kwanza za nyumbani, kwanza dhidi ya Valencia na pili dhidi ya klabu iliopo chini ya jedwali ya Levante. Lakini haikuonekana kama swala la kutia wasiwasi.
Zidane: "Hatufurahishwi na kiwango cha mchezo lakini tuna muda mwingi wa kurekebisha''.
Jumatano 20 Septemba: Real Madrid 0-1 Real Betis
Baada ya kufunga magoli katika mechi 73 mfululizo , uzoefu ulioanza miezi 17 iliopita, Real Madrid walishindwa nyumbani na Real Betis iliopo katikati ya jedwali .Hatahivyo Zidane alikuwa mtulivu.
Zidane: "Leo haikuwa siku nzuri , soka mara nyengine huwa hivyo lakini hatufai kuwa na wasiwasi''.
Jumapili, 29 Oktoba: Girona 2-1 Real Madrid
Mambo yalianza kuwa mabaya zaidi. Baada ya kufungwa na klabu iliopandishwa daraja Girona debutants Girona, Zidane alianza kukubali kwamba timu yake inadorora.
Zidane: "Ni wakati mbaya , lakini lazima ukubali .tuna timu yenye uzoefu iliojaa wachezaji bingwa na tutabadilisha hali hii"
Jumamosi, 23 Disemba: Real Madrid 0-3 Barcelona
Baada kutawaliwa na Barcelona katika kipindi cha pili cha mechi , kulikuwa na hofu kubwa kuhusu hatma ya kocha Zidane mwisho wa msimu huu ambaye timu yake ilishinda mataji matano.
Zidane: "Tuko chini kwa sababu ni uchungu kushindwa. kesho watanitimua hiyo ni kandanda , lakini haitabadilisha kile ninachofikiria ama kile ninachofanya.
Jumatano, 24 Januari: Real Madrid 1-2 Leganes
Msumari wa mwisho uligongwa katika jeneza, pale klabu ndogo ya Madrid Leganes ilipoilaza Real Madrid
Zidane: "Ni balaa . Ni kipindi changu kibaya zaidi kama mkufunzi . Nachukua jukumu la matokeo mabaya lazima nitafute suluhu''.
Kitu cha kushangaza kuhusu matokeo mabaya ya Real Madrid msimu huu ni kwamba hakuna aliyedhania kwamba klabu hiyo itafikia wakati mgumu kama huo na hakuna mtu anayeweza kuelezea.
Walikuwa wazuri sana msimu uliopita ikiwa timu ya kwanza kuhifadhi kombe la vilabu bingwa Ulaya na kushinda taji la La Liga kwa mara ya kwanza tangu 2012.
Hakujakuwa na tatizo lolote la majeraha, hakuna msuguano wowote, hakuna udhaifu wowote .lakini la kushangaza ni kwamba kundi hilo hilo la wachezaji ambalo lilishinda kila kitu msimu uliopita sasa linacheza vibaya , kibinafsi na kwa pamoja.
Pablo Brotons ni miongoni mwa wahariri wa gazeti la Marca wanaoshindwa kuelewa kushuka kwa mchezo wa Real Madrid.
''Kutoka nje ni vigumu kuchanganua kilichotokea katika chumba cha maandalizi'' , Brotons aliambia BBC Sport akiongezea ni wazi kwamba kiwango cha mchezo sio kama kile cha msimu uliopita licha ya klabu hiyo kumiliki wachezaji walewale.
Lakini ni wazi kwamba kuondoka kwa wachezaji kama vile Pepe, Rodriguez na Alvaro Morata kumeathiri timu zaidi ya ilivyotarajiwa.
Walikuwa wachezaji waliokamilisha kikosi bora zaidi. Mahala pa wachezaji hao palichukuliwa na wachezaji wadogo kama vile Jesus Vallejo, beki wa kushoto Theo Hernandez, kiungo wa kati Marcos Llorente na Dani Ceballos ambao hawajapewa fursa ya kucheza.
Tatizo la kununua mchezaji atakayejaza pengo lililowachwa na Morata limesababisha hali mbaya. Cristiano Ronaldo amefunga mabao 11 akiwa chini ya kiwango chake cha kawaida , Gareth Bale amefunga mabao sita huku mshambuliaji Karim Benzema akifunga mabao 2 pekee katika mechi 16.
Katika hali hiyo uamuzi wa kocha Zidane kutonunua wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari ulikuwa wa kushangaza na hatua yake ya kukataa kuwawacha nje washambuliaji wanaotegemewa kama vile Benzema na Ronaldo mbali na kushindwa kwake kuimarisha viwango vya mchezo wao kumemuwacha na presha chungu nzima.
Baada ya kushinda mechi 12 kati ya 22 , kubanduliwa katika kombe la Copa del Rey na klabu ya Leganes, na kufungwa na Tottenham katika uwanja wa Wembley katika kombe la vilabu bingwa , nafasi ya Real Madrid kuwashinda PSG inaowashirikisha wachezaji Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani ni chache mno.
Kulingana na mchanganuzi wa soka nchini Uhispania Julio Maldonado, kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya klabu inayoshushwa daraja ya Levante , Real Mdrid itahitaji kuimarika sio tu kuishinda PSG bali kuwa na fursa ya kufanya hivyo.
Htahivyo hili ni kombe la Ulaya na ni vigumu kuipuza Madrid katika shindano wanalohisi ni lao hususan baada ya kushinda kombe hilo mara 12.
Muhariri wa gazeti la Marca Brotons anasema kuwa '' ni kweli wanawaweza kushinda taji la klabu bingwa, ni shindano wanalopenda sana ni raundi ya muondoano na chochote kinaweza kutokea katika dakika 180.
Kumbuka kwamba 1998 walikuwa katika hali kama hiyo na wakafanikiwa kuishinda Juve mjini Amsterdam chini ya ukufunzi wake Jupp Heynckes .
Na hakukuwa na tofauti yoyote kubwa miaka minne iliopita baada ya kutocheza vizuri katika msimu wa kwanza wa kocha Carlo Ancelotti na hivyobasi kumaliza katika nafasi ya tatu , lakini bado wakaweza kushinda kombe la klabu bingwa baada ya bao la dakika za lala salama kuwasaidia kuwashinda wapinzani wao Atletico Madrid 4-1 baada ya muda wa zaida.
Kiwango cha mchezo wa Real Madrid kimeshuka, lakini bado wanaweza kuonyesha mchezo mzuri kama ilivyokuwa wakati wa ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociedad. Na katika klabu bingwa huwezi kuwapuuzilia mbali kwa sababu ni mapema mno
Rais wa Klabu hiyo Florentino Perez - huenda asimpige kalamu kocha anayeheshimiwa sana katika ulkimwengu wa soka kama Zidane huku Brotons akisema kuwa sio kocha aliyeiongoza Real Madrid kushinda mataji matano katika kipindi cha mwaka mmoja bali ni mtu anayeshimiwa sana katika klabu hiyo.
Lakini kuna uwezekano raia huyo wa Ufaransa atakubali kujiuzulu mwisho wa msimu badala ya kulazimishwa kuondoka na majina kadhaa yamewekwa kumrithi.
Mkufunzi wa Ujerumani Joachim Low ndio kocha anayeorodhshwa wa kwanza kumrithi iwapo atakubali kurudi kusimamia klabu , Meneja wa Chelksea Antonio Conte pia anapigiwa upatu iwapo atapatikana na kumekuwa na mazungumzo ya Jose Mourinho ambaye ni rafiki wa karibu wa Perez kurudi.
Mtu mmoja anayezidi kupigiwa upatu kumrithi Zidane katika Bernabeu. Majina kadhaa yapo mezani lakini jina kuu linalojitokeza kila mara ni lile la Mauricio Pochettino," kwa mujibu wa Brotons.
Raia huyo wa Argentina anaheshimiwa sana na Florentino Perez, ambaye pia amekuwa akimtaka sana Jurgen Klopp tangu kipindi chake na Borussia Dortmund .Lakini nambari moja katika orodha hiyo ni Pochettino."
Zidane huenda akaondoka na wachezaji maarufu kama vile Ronaldo na Bale huku kukiwa na mapendekezo kwamba klabu hiyo inahitaji mabadiliko.
Na tazama tena klabu ya Tottenham kwa kuwa wachezaji wanaohitajika ni Neymar na mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane. Hivyobasi huenda isiwe hatma ya Zidane inayotazamiwa bali pia ile ya Tottenham.



By:"ragbuone

No comments:

Post a Comment