Tuesday, 6 February 2018

Sure boy &Himidi:" Tuko Fiti kuikabili Simba Leo

LEO Jumatano Simba na Azam wanatarajia kukutana kwenye mchezo wao wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, uongozi wa timu ya Azam umefunguka na kusema kuwa wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mchezo huo huku ikitarajiwa kuwa na mastaa wao Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ na Himid Mao.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofi sa Habari wa  zam, Jaff ar Idd, alisema kuwa wanawajua wapinzani wao lakini hata wao wana kikosi kipana na wanataka kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuweza kuwa kwenye nafasi nzuri na baadhi ya wachezaji wao ambao mchezo wao uliopita waliukosa watakuwepo.

“Kesho (leo) tuna mchezo dhidi ya Simba na pointi tatu ni muhimu kwetu kwani mwalimu Cioaba ameshakiandaa kikosi kamili tayari kwa ajili ya mchezo wetu.

“Hii ni raundi ya lala salama kama usipochanga karata zako mapema basi utashindwa kuhusu Salum Aboubakar (Sure Boy) atakuwepo kwani adhabu yake ilishamalizika na kikosi kina majeruhi wawili tu ambao ni Waziri Junior pamoja na Joseph Kimwaga, wote waliobaki watakuwepo akiwemo nahodha Himid Mao,” alisema Jaffar.

No comments:

Post a Comment