Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa Sudan kuisni nchini Ethiopia yamegonga mwamba kwa baada ya wajumbe kususia kikao hicho, Radio Tamazuj inaripoti.
Hii ikiwa ni jitihada ya hivi karibuni kusitisha mapigano ya kiraia yaliodumu zaidi ya miaka minne mpaka kufikia sasa.
Kituo hicho cha utangazaji kinasema ujumbe wa serikali ulitaka zaidi ya wajumbe watatu wahudhurie kikao hicho. Pande hizo mbili zinatarajia kufufua makubaliano ya amani ya mwaka 2015.
Duru tofauti mjini Addis Ababa zimeiambia Radio Tamazuj kwamba ujumbe wa serikali uliamua kususia kikao cha leo mchana kwasababu walitaka zaidi ya wajumbe watatu kuhudhuria.
"Serikali inataka wajumbe zaidi ya watatuu wahuhudhurie lakini IGAD inaruhusu watau pekee," mmoja wao alisema.
Kikao cha pili leo mchana kinafafanua kuhusu ajenda ya awamu ya pili ya mpango wa kufufua makubaliano ya amani ya mwaka 2015.
Sudan Kusini yaonywa kukumbwa na maafa
Sudan Kusini yaua raia wake
Mazungumzo hayo yanajiri katika wakati ambapo kunajumuiya ya imatiafa inazidi kushindwa kuuvumili utawala wa kisiasa na kijeshi wa taifa hilo changa barani Afrika.
Wajumbe wa Sudan Kusini walipewa ujumbe mkavu muda mfupi kabla ya kutarajiwa kaunza kikao hicho. Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, aliwaambia kwamba wanahusika kwa jinamizi wanalolishuhudia hivi sasa raia wa Sudan kusini.
Makubaliano ya mwisho ya kusitisha mapigano yalitiwa saini mkesha wa Krismasi na ulidumu kwa saa kadhaa.
Katika miaka minne iliyopita, maelfu ya watu wameuawa katika mapigano na kiasi ya thuluthi moja ya raia nchini wameachwa bila ya makaazi.
Marekani iliunga pakubwa mkono uhuru wa Sudan kusini mnamo 2011.
Lakini wiki iliyopita Marekani iliidhinisha vikwazo vya silaha na hivi karibuni mkuu wa muungano wa Afrika ameitisha kuidhinisha vikwazo dhidi ya wanaorefusha mzozo huo.
Tuesday, 6 February 2018
Mazungumzo ya Sudani kusini ya gonga Mwamba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment