Wednesday, 7 February 2018

Part 2:""TUNDULISSU :"LEMUTUSI usilazimishe urafiki

2. LEMUTUZ ASILAZIMISHE URAFIKI USIOKUWEPO!!! .

Kwa wasomaji wa story ya mwanzo basi kama Atamalizi na Hii zairi shairi Atakuwa amefika Muafaka wa jambo hill kwa upande wa TUNDULISSU sasa endeleae 👇👇


""""""""Kama Lemutuz, wengi wa niliyopiga nao picha nilikuwa siwafahamu kabisa kabla ya kukutana nao siku hiyo. .

Tatu, tangu siku hiyo sijawahi kufanya mawasiliano na Lemutuz ya aina yoyote. Nakumbuka tu kukutana na kusalimiana nae bungeni mwaka 2012, wakati alipokuja Dodoma akitaka kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. .

Mimi sijajua sababu ya Lemutuz kutaka kulazimisha urafiki na mimi usiokuwepo. Yeye ni rafiki mkubwa wa Bashite na mpiga debe wa Rais Magufuli. .

Mimi ni mpinzani mkubwa wa Magufuli na nimelipa gharama kubwa kwa sababu ya msimamo wangu tangu Magufuli aingie madarakani. .

Huo 'urafiki mkubwa' unaodaiwa kuweka kati yangu na Lemutuz msingi wake ni nini???
.

Mwisho, ukitaka kuongopa hadharani basi angalau uwe na kumbu kumbu sahihi. Lemutuz anadai tulikutana 2010 wakati ilikuwa Mei 2011. .

Anadai nilikwenda kwenye graduation ya dada yangu (ambaye hata jina hakumtaja!) wakati ilikuwa graduation ya kaka yangu Vincent Mughwai. .

Anadanganya ilikuwa Connecticut State University wakati ilikuwa Bridgeport University. Anadai alinipokea JFK wakati nilipokelewa na kaka yangu Vincent. .

Na tangu nimepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na wanaoitwa 'watu wasiojulikana', rafiki yangu mkubwa huyu hajawahi kunitumia hata kadi ya pole!!! .

Huu ni urafiki feki wa kuwadanganyia Watanzania wasioelewa. .

Msidanganyike!!!

No comments:

Post a Comment