Monday, 5 February 2018

ANTONIO CONTE:"Chelsea amueni chochote Niko tayari sasa ivi!

Katika moja ya mkutano na waandishi wa habari ambao ulionekana kugubikwa na hisia sana ni usiku wa kuamkia leo wakati Antonio Conte akizungumza baada ya mchezo wao dhidi ya Watford kumalizika.           Chelsea walidhalilika tena kwa kupigwa bao 4 kwa 1 jambo ambalo limeendelea kuwasha moto Stamford Bridge na sasa kocha wao Antonio Conte yuko katika kitimoto huku hatma ya kibarua chake ikiwa kwa Roman Abromovich.Lakini Conte yeye amesema suala la kazi anawaachia mabosi wake kwani yeye binafsi amekuwa akijitoa kwa 120% kwa ajili ya timu hiyo na kinachotokea uwanjani ndio kama hivyo kinavyoonekana.Conte amesema kuhusu kibarua chake yeye anaona yuko poa tu na Chelsea lakini kama wenyewe Chelsea wataona kwamba hafai kuendelea kukaa klabuni hapo baasi ataondoka tu lakini hana wasiwasi.Antonio Conte amesisitiza kwamba yeye hakoseshwi usingizi na tetesi za kufukuzwa kazi na amesema yeye anaona anafanya vizuri kwa ajili ya Chelsea ila kama wataona vinginevyo baasi watafanya lililo sahihi.Conte inasemekana alijaribu kuongea na uongozi wa Chelsea kabla ya mchezo wao na Watford kuhusu kujaribu kuongea na wanahabari kuhusu uhakika wa kibarua chake lakini Chelsea hawakuwa tayari kwa sasa kuongelea hilo.Mara ya mwisho kwa Chelsea kukubali kipigo mfululizo cha mabao 3+ katika EPL ilikuwa mwaka 1995 walipopigwa na United 1-4, kisha wakapigwa na Blackburn 0-3, kwa hiyo jana inakuwa mara ya kwanza kufanywa hivyo tangu 1995.

No comments:

Post a Comment