Esmond Bradley Martin, mojawapo ya wachunguzi wakuu duniani dhidi ya biashara haramu ya kimataifa ya pembe za tembo na vifaru, amepatikana amedungwa kisu na kuuawa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Alifanya uchunguzi wa siri katika baadhi ya maeneo hatari na magumu duniani, akipiga picha na kuorodhesha masoko ya pembe hizo, akizungumza na walanguzi, na kufanya hesabu za bei katika soko haramu la biashara hiyo yote katika jitihada za kuwaongoza waundaji sera katika uhifadhi wa mzingira.
Katika miaka kadhaa ya nyuma, alisafiri kwenda China, Vietnam na Laos na mratibu Lucy Vigne, wakifika katika maeneo ambayo watu wachache wa mataifa ya nje wangesubutu kuyakanyaga, wakijifanya kuwa wanunuzi wa pembe za tembo na vifaru.
Katika eneo la kucheza kamari linalomilikiwa na Wachina huko Laos, wapenzi hawa wasio wa kawaida walipishana na majangili, walanguzi wa madawa ya kulevya, na waendesha biashara haramu ya kusafrisha watu , silaha na wanyama pori ili kuweza kupata data.
Utafiti wao uliofadhiliwa na shirika la Save the Elephants, umefichua kuwa Laos limekuwa eneo linalokuwa haraka la biashara ya pembe hizo duniani.
Walikuwa wamerudi hivi maajuzi kutoka safari nchini Myanmar na bwana Martin alikuwa anaandika taarifa alizokusanya wakati alipouawa.
Polisi wanachunguza chanzo cha kuuawa kwake. Alifariki kutokana na kudungwa kisu shingoni nyumbani kwake karibu na Kren nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.
Inaonekana kana kwamba ulikuwa ni wizi wa mabavu uliokwenda sege mnege, lakini polisi wanachunguza iwapo kifo chake kinahusiana na kazi aliyokuwa anafanya.
Katika mahojiano na BBC mnamo 2016, alisema kuwa sababu ya kuongezeka kwa uwindaji haramu katika miaka mitano iliyopita barani Afrika ni kutokana na usimamizi mbaya wa maeneo ambayo tembo wanaishi.
"Huenda rushwa ndio chanzo kikuu cha kuongezeka kwa uwindaji wa Tembo. Rushwa katika viwango vyote," alisema.
"Kilichotokea katika miaka michache iliyopita ni kwamba raia wengi wa Uchina wameingia Afrika.. kuna pengina takriban raia milioni moja au hata zaidi wa CHina wanaofanya kazi sasa Afrika.
"Tuliochonacho ni masoko makubwa yalio wazi ya haramu ya pembe hizo katika nchi kama Angola, Nigeria, Misri, Sudan - na Msumbiji, nadhani - na pembe nyingi kutoka maenoe hayo hununuliwa na Wachina."
Alisaidia kufungwa kwa masoko hayo mengi ya wazi - na kuzifanya serikali zilizo na rekodi duni za uhalifu wa wanyama pori, zizinduke.
Biashara ya pembe za Faru halali Afrika Kusini
Jinsi pembe za faru hugeuzwa kuwa vito na kusafirishwa ng'ambo
Kazi yake huko China imepigia upatu pakubwa kwa kusaidia kuhimiza kupigwa marufuku ya uuzaji wa ndani ya nchi wa pembe za tembo mwaka huu - na uuzaji wa pembe za vifaru katika miaka ya 90.
Alijua kuvaa
Nywele nyeupe kama theluji na suti iliyokamilika, kwa kawaida hakosi kitambaa cha mkononi kinachoning'inia kutoka mfuko wake wa koti.
Esmond Bradley Martin alikuwa hana maneno mengi, lakini n mtu mwenye malengo, mchangamfu na hujishughulisha kikamilifu na kazi yake - kukusanya data na taarifa kuhusubiashara haramu ya uwindaji wa wanyama pori.
Alizaliwa New York, aliwasili Kenya kwa mara ya kwanza katika miaka ya 70 wakati Tembo walikuwa wanauawa kwa ajili ya pembe zao kwa idadi kubwa.
Ni wakati huo ndipo alipokutana na muasisi wa shirika la Save the Elephants, Iain Douglas-Hamilton, ambaye anasema kifo cha rafiki yake wa miaka 45 ni pigo kubwa mno kibinfasi na ki taaluma.
"Esmond alikuwa ni mojawapo wa mashujaa wa uhifadhi wa mazingira ambaye hakuthaminiwa ipasavyo," anasema.
"Kazi yake kubwa dhidi ya masoko haramu ya pembe za Tembo na vifaru aliifanya katika maenoe hatari kwa mara nyingi na dhidi ya harakati nyingi ambazo zinaweza kwa kawaida kumchosha mtu aliye na nusu ya umri wake.
"Wakati wa miaka 18 ya kazi yake na Save The Elephants, Esmond - pamoja na watafiti wenzake - wamechapisha ripoti kumi dhidi ya masoko halaili na ya haramu ya pembe za Tembo."
Mhifadhi mazingira wa Kenya Paula Kahumbu anasema bwana Martin kwa kawaida alikuwa hafichi taarifa za utafiti wake na alikuwa akisambaza aliyoyagundua kwa manufaa makubwa.
"Alikuwa mbele ya kila mtu katika kutambua namna biashara ya pembe za Tembo na Vifaru inavyoendeshwa ," anasema, akigusia utafiti wa hivi karibuni wa bwana Martin.
"Kutambua kuwa biashara hiyo imesogea kutoka Uchina hadi katika nchi jirani itasaidia wanamazingira kuzishinikiza serikali kufanya mageuzi."
Kuna mgawanyiko katika jamii ya wahifadhi mazingira kuhusu mtazamao upi ulio bora katika kuwaokoa Tembo na vifaru: Kuruhusu na kuratibu biashara hiyo ili kupata kipato, au kupiga marufuku kabisaa biasharanzima na bidhaa haramu ili kubadili mitazamo.
Balozi wa Marekani Kenya, Bob Godec, amelaani mauaji ya Martin na kusema ni mkasa mbaya kwa Kenya na dunia.
Anasema binafsi atakosa busara, ufahamu, na na upendo aliokuwanao wa kazi yake, akiongeza: "Wanyama pori barani Afrika wamempoteza rafiki wa kweli, lakini kazi zake katika uhifadhi wa mazingira utaendelea kwa miaka inayokuja."
Tuesday, 6 February 2018
Home
/
Unlabelled
/
ESMOND BRADLEY MARTIN:" Mchungaji aliyejitoa muanga wa kuwakabili wawindaji haramu auawa Kenya..
ESMOND BRADLEY MARTIN:" Mchungaji aliyejitoa muanga wa kuwakabili wawindaji haramu auawa Kenya..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment