Thursday 1 March 2018

SHILOLE Mahakaman kwa Utaperi

Msanii wa mzuki wa kizazi kipya nchini, zuwena mohamed maarufu kama shiloleh amefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuchukua pesa ya shoo kiasi cha shilingi milioni 3 ikiwa ni pesa aliyokuwa amelipwa kwa ajili ya kufanya shoo lakini siku ya tukio msanii Shiloleh alishindwa kuonekana katika shoo hiyo na kushindwa kutoa taarifa kwa waandaji wa shoo hiyo  kwa muda muafaka,hivyo kusababisha hasara.
Shiloleh amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo manispaa ya Kinondoni leo na kupewa hukumu ya shilingi mil 14, ikiwa ni pamoja na fidia ya kumsababishia hasara Mama Mary Musa aliyemlipa kwa ajili ya kufanya shoo siku ya pasaka mwaka 2017 Mbagala Kijichi ambapo baada ya kulipwa alishindwa kufika ukumbini hapo kwa muda hivyo mashabiki na wapenzi wa burudani kushindwa kuvumila na kupandwa nahasira iliyosababisha kuvuja na kuharibu mali.
Kwa mujibu wa GPL, shiloleh alipofanya kosa hilo alitakiwa kurudisha pesa hizo lakini alikuwa akipuuza agizo hilo la mahakama kwa muda wote ndipo mama huyo alipoamua kufatilia zaidi na hukumu kutolewa leo kuwa ndani ya wiki moja Shiloleh anapaswa kulipa fidia hivyo na kama hatashindwa basi mali zake zitashikiliwa na mahakama.
Shiloleh amefika mahakama hapo akiwa na mume wake uchebe lakini baadae alianza kuangu akilio baaada ya hukumu kutolewa.

No comments:

Post a Comment