Friday 16 February 2018

RAYVANNY :" aanika mkwanja anaolipwa WCB!


MSANII anayefanya poa kutoka Crew ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Rayvanny ametumia muda wake kukaa chini na The One na kuelezea utaratibu mzima unaotumiwa na bosi wao Diamond Platnumz kuwalipa mishahara na posho kadhaa zinazotokana na shoo ambazo wamekuwa wakizifanya.

Akizungumza na Global Entertainment, alisema kuwa Crew hiyo imekuwa ikilipwa vizuri mishahara huku ikiwataka wasanii wake kuingiza kiasi flani cha fedha wanazopata katika shoo zao kwenye mfuko wa kampuni tofauti na bosi wao Diamond ambaye hakatwi hata senti ya shoo.

“Kutokana na maisha mazuri ya WCB, ndiyo maana utaona siku hizi anaweza kuibuka msanii wake yoyote na kutoa ushuhuda juu ya kiasi cha fedha ya maisha anayoipata,  jambo ambalo baadhi yao wanaona kama majigambo lakini uhalisia unabaki kuwa kweli maisha ndani ya WCB siyo mabaya.

“Suala la Harmonize kusikika akisema ana fedha, huo ulikuwa kama ushuhuda wake kwani kila mtu ana njia yake ya kushuhudia jambo ambalo anatendewa au alilokuwa akitendewa katika maisha yake ya nyuma au anayoendelea kuyaishi kwa sasa,” alisema Rayvanny.

No comments:

Post a Comment