Monday, 5 February 2018

Japokuwa kwenye soka wanasema mpira huwa unadunda lakini kwa Jose Mourinho ni kama vile amekubali tu mambo yaishe na kuamua kuwapa Man City ubingwa wa EPL msimu huu.
United wana alama 53 ikiwa ni alama 15 nyuma ya City na Jose Mourinho sasa amewataka vijana wake kupambana ili msimu ujao wa ligi waweze kuchukua kombe la ligi kuu.
Mourinho amesema kwa sasa anafurahia kiwango cha wachezaji wake na anafurahia kwamba msimu huu kuna mabadiliko makubwa uwanjani tofauti na msimu uliopita.
Amesema watajaribu kuwa “wakwanza wa wamwisho”(wa pili) japo pia sio jambo rahisi kwani Liverpool, Chelsea na Tottenham nao wanaonekana wanaweza kukaa katika nafasi hiyo.
Mourinho amemsifu Pep Gurdiola kwa kile anachofanya hivi sasa ambapo anaoneka hataki kuachia timu nyingine zimkaribie, jambo ambalo linaenda kumoa ubingwa hivi karibuni.
Manchester United wanakwenda kuikaribisha Huddersfield hii leo katika dimba lao la Old Traford mchezo ambao utakuwa sehemu kuelekea kumbukumbu ya tukio ajali ya ndege iliyotokea Ujerumani mwaka 1950 ambapo Jumatano ya tarehe 6 ndio kumbukumbu yenyewe.

Comments

No comments:

Post a Comment