Ni kawaida ya watu wengi wakiamka asubuhi kukimbilia simu zao lengo kubwa ni kuangalia message na kupitia mitandao ya kijamii, ila leo kwa mara ya kwanza nimeamka na kufungua YouTube moja kwa moja kuangalia trailer la Black Panther si walitangaza linatoka kwenye game 4 ya fainali za NBA na hapo hata matokeo sikuwa na hamu nayo.
Black Panther ni comic book ya pili niliyoisoma sana baada ya The Walking Dead namkubali sana na ndio super hero ninayemkubali kuliko wote ukitaka kubishana nitafute muda mwingine. Hebu tuanze moja kwa moja uchambuzi wetu.
Trailer linaanza tunamuona Andy Serkis anayeigiza kama Ulysses Klaw akiwa amekamatwa huku akihojiwa na Martin Freeman anayeigiza kama Everett K. Ross. Klaw anajaribu kumuelezea hali halisi ya nchi ya Wakanda nchi ambayo watu wengi duniani wanaihesabu kama moja ya nchi za kawaida za Afrika lakini kiuhalisia ni nchi iliyoendelea kiteknolojia kuliko zote duniani yaani kwa kifupi Marekani hawafikii teknolojia yao Tony Stark (Iron Man) na fujo zake zote hafui dafu hapa.
Wakati mahojiano yakiendelea tunamuona King T’challa/Balck Panther akiwa na Okoye (Danai Gurira, The Walking Dead) kiongozi wa kikosi cha ulinzi cha mfalme kinachoundwa na wanawake watupu kiitwacho Dora Milaje (The Adored Ones) wakiangalia kinachoendelea kabla ya Erik Killmonger kuvamia na kumuokoa.
Hapa tunapata nafasi ya kuona mandhari ya nchi ya Wakanda na tukimuona Black Panther akiingia kwenye uwanja kama kwa ajili ya matambiko yanaweza kuwa ya kuapishwa kuwa mfalme. Na kwa wananchi wa Wakanda sio kisa wameendelea ndio wanaacha asili jina lingine la Black Panther ni King of Dead kwani anaweza kuongea na Black Panther waliokufa wa miaka ya nyuma.
Na hapa tunazidi kuona madhari zaidi ya Wakanda, usishange hiyo ni Afrika na hapa director fundi na kijana mdogo kabisa Ryan Coogler na timu yake wanafanikiwa zaidi kuchanganya mandhari ya kiafrika na teknolojia na kutoa picha yenye muonekano wa pekee kabisa. Kama unataka kusoma vitabu vya Black Panther unaweza ukaanza na mwendelezo wa vitabu vya sasa hivi unao andikwa na Ta-Nehisi Coates kwani vitu vingi kwenye movie hii vimetoka huko, ukitaka kuona ramani ya Wakanda ili kujua iko wapi Afrika angalia mwisho wa makala hii.
Kwa wale wapenzi wa Hollywood wanamfahamu mwanamama Angela Basset hapa anaigiza kama Ramonda, Malkia na mama wa Wakanda na pia ni mama wa kambo wa T’challa, hapa yuko na Lupita Nyong’o pamoja na Everett Ross kwenye eneo la milima nchini kama wanakimbia hatari fulani hivi.
Huyu ni Shuri ni dada mdogo wa kambo wa T’challa na princess wa Wakanda hapa anaigizwa na muigizaji kutoka Uingereza aitwaye Letitia Wright na hapa tunamuona akitumia glovu za mizinga za panther, huyo kwenye comic kuna kipindi alishawahi kuwa Black Panther kwa kifupi yuko vizuri pia, na yeye pia kama walivyo watu wengi wa Wakanda ni mwana sayansi ambaye amebobea kwenye teknolojia ya vibranium na huitumia hasa kwenye ku-design mavazi na silaha za Wakanda.
Maadui wa movie hii ukiachana na Ulysses Klaw anayeonekana amekamatwa mwazoni kabisa pia yupo Erik Killmonger anayigizwa na Michael B. Jordan walioiona movie ya Creed watakuwa wanamkumbuka. Vita kati ya Black Panther na Killmonger na vya binafsi kwani inasemakana baba yake alilazaimishwa kumsaidia Klaw kuiba vibranium hapo mwanzoni iliyopelekea kwa familia kufukuzwa nchini humo. Ugomvi wake ni kati na familia ya kifalme akiwa na lengo la kuipundua na yeye kama alivyo Black Panther ni mwana sayansi, genius na anajua kupigana pia akiwa na mbinu za hatari.
Hapa tunamuona Killmonger akiwa kwenye vazi lake tayari kwenda kumuokoa Klaw na picha ya hapo juu anaonekana amekamatwa na kama utaangalia pembeni yake utamuona Daniel Kaluuya kwa wale walioangalia movie ya Get Out watamkumbuka, hapa anaigiza kama W’kab, kiongozi wa ulinzi wa nchi ya Wakanda.
Adui mwingine atakayekuwepo huku ni M’baku kabla akijulikana kama Man-Ape, nafasi hii inaigizwa na Winston Duke kwa wapenzi wa series ya Peson of Interest watakuwa wanamkumbuka Dominic.
Hapa inaonekana kama M’baku amefanikiwa kuwateka Queen Ramonda na walinzi wake akiwemo pia Everett K. Ross.
Hapa tunamuona Lupita Nnyong’o hapa akiigiza kama Nakia mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi cha King T’challa cha Dora Milaje akiwa kwenye Cassino akipeleleza watu fulani
Wanajeshi wote kikosi cha ulinzi cha Dora Milaje yaani bodyguard wa Black Panther ni wanawake watupu kama marehemu Gaddafi vile. Hawa ni mabinti kutoka katika kila kabila nchi ya Wakanda wanaletwa kwenye kasri ya kifalme wakiwa wadogo wanafundishwa mambo mengi sana hasa kwenye mapigano na ni moja ya wapiganaji hatari kwenye nchi nzima, lengo la wao kuchaguliwa kutoka kila kabila nchi humo ni kuzuia watu wa makabila hayo kushambulia ufalme kwani wao wamefundishwa kufa kwa ajili ya mfalme na mtu yeyote ndani ya nchi akishambulia ana nafasi kubwa ya kumuua ndugu yake. Wana historia ndefu tunaweza kuichambua siku moja.
Niliahidi ramani ya Wakanda unaliona ziwa Victoria jamaa ni ndugu zetu kama huna habari