Wednesday 24 October 2018

REVIEW| Vitu ambavyo hauja gundua katika movie ya Apocalypto [Soma hapa]

Leo nawapa Story fupi kabisa ila kuhusu movie moja bora na iliyopendwa Sana hadi Leo hii movie ukikaa na kuitazama basi hapana Shaka bado ina utamu wake ule ule na msisimuko uleule ambao bado haujapotea japokuwa ni movie ya zamani kidogo 

Apocalypto (Maana Kwa Kiswahili: Mwanzo Mpya) Ni Jina La Filamu lliyo Tengenezwa Chini Ya Muongozaji Hodari Mel Gibson

Mel Gibson, Anasema Filamu Hii llitokana Na Wazo Kwamba Kijana Mmoja Anakimbizwa Na Kundi La Wahuni. Wakati Anakimbia Kuokoa Maisha Yake Pembezoni Mwa Ufukwe Wa Bahari Anakutana Na Christopher Columbus Na Kundi Lake. Ikumbukwe Kwamba Jamii Ya Wa Mayans Ndio Walikua Watu Wa Kwanza Kukutana Na Kundi La Watu Toka Ulaya (Akina Columbus) Mnamo Mwaka 1502. Hapo Ndipo Akapata Wazo La Kila Tulichokiona Ndani Yake. Sasa Sikia Hii
1: Mnyama Anayefukuzwa Pale Mwanzo Wa Movie Sio Nguruwe Kama Wengi Tunavyodhani, Bali Ni Tapir. Tapir Ni Aina Ya Mnyama Ambaye Alipatikana Katika Maeneo Ya Kusini Na Kati Kati Ya Latin America. Yeye Ndiye Alikua Mnyama Mkubwa Zaidi Kipindi Kile Cha Miaka Ya 1511 Kwa Sababu Punda Na Farasi Walikua Bado Hawajaletwa Na Wa Spain
2: Katika Uchukuaji Wa Vipande Vya Filamu Hiyo Inasemekana Kwamba Kuna Ng’ombe Alianguka Katika Maporomoko Ya Maji (Waterfalls) Yenye Urefu Wa Futi 170 Toka Juu Hadi Chini, Kiasi Kwamba Crew Nzima Ya Apocalypto Walihisi Kwamba Yule Ng’ombe Kafa, Lakini Cha Ajabu Alinyanyuka Na Kutoka Mle Mtoni Kisha Akaaaza Kula ‘Majani Kama hakuna Kilichotokea…!!! Maajabu

By R_one Library online 



No comments:

Post a Comment