Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts
Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts

Thursday 18 October 2018

Dalili kumi (10) za mwanamke anae kupenda hizi hapa [Soma zote]


Karibu mdau wangu uweze kujifunza na R ONE  Leo nimekuandalia Dalili 10 ambazo atazionyesha mwanamke anae kupenda ila ana shindwa kukuambia nazo ni Kama zifuatazo 
1. Atakutega kupata attention yako. Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au lah! Mf wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na kuangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake au

2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe

3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli

4. Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.
 
5. anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatowez kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza

6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiais gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia.
Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.

7. Hupenda kukaa mmuda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe.

8. Yupo tayari kuangamiza. Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwamba hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine. 
9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake. Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.

10. Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose

Friday 10 August 2018

MAMBO 8 YANAYO MTOKEA MWANAMKE HASIPO FANYA MAPENZI MUDA MREFU

Yawezekana huna mpenzi au labda huna muda wa kutafuta mwenza, utakapoona mabadiliko haya mwilini mwako basi inabidi ufikirie kuanza kale kamchezo ketu. Haya ni mabadiliko yanayoweza kutokea mwilini mwako utakapoacha kufanya mapenzi, na si mabadiliko mazuri kama namba hili la kwanza katika mabadiliko haya:
1. Unaweza kupata ndoto nyevu

Kama inavyomtokea mtoto wa kiume aliye kwenye balehe, wanawake wasiofanya mapenzi mara kwa mara, watajikuta wakipata ndoto nyevu wakiwa usingizini.hii itakutokeasio tu kwa kutokufanya mapenzi mara kwa mara bali hata unapoacha kupiga punyeto.
Wanawake wengi wanakosa uhakika kama wanapata ndoto nyevu kwa kuwa inategemea endapo atakumbuka, kwakuwa hakuna kumbukumbu nyepesi kuisahau kama kukumbuka ulichoota.
Haikuwa rahisi kwa watafiti kuwa na jibu kuhusu kusisimka kwa mwanamke akiwa usingizini, kwakuwa inabidi wapime mapigo ya moyo, kupima ubongo na kufatilia mabadiliko ya joto ukeni.
2. Unapoteza hamu ya kufanya mapenz

Japokuwa usemi wa “usichokitumia kitapotea” unatumika kuelezea jambo kama hili, wanawake hawapotezi kitu chochote ambacho hakiwezi kurudi kwenye hali yake ya kawaida, walau wakiwa katika hatua za kuweza kupata watoto. Ni kawaida sana kwa mwili wa mwanamke kuacha kuwaza kufanya mapenzi kama hakufanya kwa muda mrefu. Mwili unazoea hali ya kutopata hisia hizo.
Hamu ya kufanya mapenzi inaweza ikapotea, kitu ambacho sio kibaya sana kama unataka kufanya mambo mengine. Pia utaweza kuachana na mambo yanayotokana na hisia zako za mapenzi. Kama hutaki kupoteza hamu ya kufanya mapenzi hata kwa muda kidogo, kujichua kunaweza kukusaidia hili. Mshauri wa masuala ya kujamiiana Holly Richmond, ambaye ni Daktari wa Saikolojia ya ufanyaji kazi wa mwili wa binadamu anasema, “Watu ambao huwa wanapiga punyeto huwa wana uwezo mkubwa wa kufikiria na ni wakarimu kwa wapenzi wao,” kwahiyo mwanamke asione aibu kupiga punyeto!
3. Kuta za uke zinadhoofika

Inafahamika kwamba ukiwa na umri zaidi ya miaka 50 hivi wanawake wanakuwa katika uwezekano mkubwa wa kutopata raha kabisa wakati wanafanya mapenzi iwapo hawatakuwa wakijamiiana mara kwa mara. Kwa kawaida, kuta za uke zinakuwa nyembamba na kudhoofika hadi mara nyingine kuanza kuchanika wakati unaingia kipindi cha ukomo wa hedhi, hali inayofanya tendo la kujamiiana liwe na maumivu makali sana. Jambo pekee la kuzuia hili lisitokee kimsingi ni kuendelea kufanya mapenzi mara kwa mara hata katika umri wako wa kustaafu. Dkt. Streicher ameliambia jarida la Reader’s Digest kwamba kupungua kwa kuta za uke kunatokana na kutopata kwa damu ya kutosha, tatizo linaloweza kurekebishwa kwa kusisimuliwa kimapenzi na kujamiiana.
“Wanawake wenye umri mkubwa ambao hawafanyi mapenzi mara kwa mara wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupungua na kufa kwa tishu za kuta za,” amesema. “Kisababishi kikubwa cha tatizo hili ni kupungua kwa mzunguko wa damu, na inajulikana kwamba kufanya mapenzi mara kwa mara kunaongeza mzunguko wa damu maeneo hayo.”
Na kama maumivu makali wakati wa kujamiiana yatakuwa hayatoshi, madhara yanayoletwa na kupungua kwa kuta za uke ni ugumu wa kutengenezwa kwa kilainishi asilia kwenye maumbile yako, jambo linalofanya kitendo cha kufanya mapenzi baada ya muda mrefu kusababisha ukavu wa hali ya juu. Ili kuzifanya kuta za uke ziwe nene na zenye afya, angalau soma vitabu vya mapenzi kila mara, na angalau uwe unapiga punyeto. Kwa muktadha kama huu ndio madaktari wakasema kuwa kama usipotumia kiungo fulani basi kitadhoofika, kwahiyo njia rahisi zaidi ya kuondoa tatizo hili ni kufanya mapenzi mara kwa mara! Mtaalamu wa magonjwa ya wanawake, Dkt. Barb DePree anasema, “Ninamhudumia mwanamke mwenye umri wa miaka 75 ambaye anasema kuwa anafanya mapenzi mara mbili kila wiki,” kwahiyo hakuna sababu ya msingi ya kutofanya.
4. Unaongezeka uzito wa mwili

Kufanya mapenzi ni njia bora sana ya kuishughulisha moyo na misuli bila kupata maumivu unayopata ukikimbia au gym. Unaweza usiwe unajua ni kiasi gani cha ‘kalori’ unakipunguza unapofanya mapenzi, lakini unaweza kugundua hilo baada ya kumaliza. Jarida la “Woman’s Day” lilichapisha kuwa kiwango cha kawaida cha kalori unachopunguza wakati wa kuandaliwa, matokeo yaliyowastua wengi. Ukiwa unapata mabusu ya kawaida tu, unapunguza kalori 68 kwa saa, lakini yanapofanywa kwa muda mrefu zaidi yanapunguza kalori zipatazo 476 kwa saa. Hii ni kwa sababu kiwango cha kupumua kinapoongezeka, kalori zinapungua kwa wingi zaidi!
Tendo la kufanya mapenzi linasaidia kuchoma kalori 144 kwa kiwango cha chini. Kiasi hiki kitaongezeaka zaidi endapo utakuwa na ushirikiano wa kutosha. Hii inamaanisha utapunguza kalori angalau 1,200 kama utakuwa unafanya mapenzi mara tatu au nne kwa wiki, kiasi ambacho ni kikubwa sana kama utakuwa hufanyi kwa muda mrefu. Kwahiyo, kama ukiacha kufanya mapenzi, utaona mwili ukianza kuongezeka uzito kidogo kidogo.
5. Kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili

Kufanya mapenzi mara kwa mara kuna faida kubwa kiafya, na tunapoacha kwa muda mrefu tunajiweka kwenye hatari ya kuugua kirahisi zaidi! Kwa mujibu wa wataalamu wa Kliniki ya Mayo nchini Marekani, kila mara mwanamke au mwanaume anapopandishwa hamu ya kufanya mapenzi, mwili unatoa homoni aina ya Dehydroepiandrosterone (DHEA). Homoni hii inasaidia kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili, ikiusaidia mwili kupambana na bakteria, virusi na vijidudu vingine vingi. Lakini faida hii itapatikana endapo mwenza wako ataweza kufika kileleni mara kwa mara.
Japo kutofanya mapenzi haina maana kwamba utapata magonjwa makubwa ghafla, kinachomaanishwa ni kwamba utakuwa unakosa faida hizi zinazotokana na kufanya mapenzi mara kwa mara. Homoni hii ya DHEA pia inasemwa kuwa inasaidia kuondoa msongo wa mawazo, kung’arisha ngozi, kurekebisha tishu zilizoharibika kwa haraka zaidi na pia kuongeza kiwango cha uelewa na kujifunza.
Utafiti uliofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu pia umebaini kiwango kikubwa cha protini aina ya immunoglobulin A, kiambata muhimu sana katika kinga ya mwili – kwa wanaofanya mapenzi walau mara mbili kwa wiki ikilinganishwa na ambao hawafanyi!
6. Kuwa na msongo wa mawazo

Sio tu kwa sababu ya raha unayopata wakati wa kufanya mapenzi, mbegu za kiume ni moja ya vinavyopunguza msongo wa mawazo kwa mwanamke. Yawezekana ikaonekana hiki ni kitu ambacho mwanaume atasema ili alale na mwanamke, lakini ndio ukweli wenyewe! Jarida la Psychology Today limeripoti kuwa katika utafiti uliohusisha wanawake 293 kuhusu tabia zao kwenye mahusiano, kama idadi ya kufanya mapenzi na iwapo wanatumia kinga au la. Kisha wakapimwa kujua viwango vyao vya msongo wa mawazo.
Ilibainika kuwa waliokuwa wanafanya mapenzi bila kinga hawakuwa na msongo wa mawazo ikilinganishwa na waliokuwa wanatumia kinga au ambao hawakufanya kabisa. Viambata vinavyopunguza msongo wa mawazo vilivyopo kwenye mbegu za kiume vikinyonywa na kuta za uke, vinamfanya mwanamke itulie kabisa! Hii ndiyo sababu watu hupata msongo wakiachana na wapenzi wao.
Kwa mujibu wa jarida la “Psychology Today,” homoni za endorphin zinazotoka wakati wa kufanya mapenzi zinasaidia kuondoa wasiwasi. Kwahiyo, unapopita muda mrefu bila kufanya mapenzi, unaweza kuona unapata msongo wa mawazo. Haijaelezwa endapo homoni hizi zinatoka iwapo utafikia kileleni au la, na ikiwa ndivyo, basi wanawake wengi hawapati faida hii kwakuwa wengi wao hawafiki. Uzuri ni kwamba hata ‘mazoezi’ unayofanya wakati wa kufanya mapenzi husaidia kufikia faida hiyo.
Tafiti moja imeonesha kuwa kwa wanaofanya mapenzi baada ya kila wiki mbili wana uwezekano mdogo wa kupata shinikizo la damu ikilinganishwa na wasiofanya kabisa au wanaopiga punyeto au wanaofanya njia yoyote isiyohusisha kujamiiana. Kwahiyo, hata ‘ukijihudumia’ mwenyewe haitasaidia sana kukupunguzia msongo wa mawazo. Kwa sababu hii, wanawake wanahitaji hasa kuwa na mwenza.
7. Unapunguza uwezekano wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, UTI na mimba usizotarajia

Mara nyingine maambukizi yanatokana na kutojikausha vizuri au kuwa na unyevu kwa muda mrefu au kuvaa nguo zinazobana sana, lakini kutofanya mapenzi inamaanisha hutakuwa na wasiwasi tena kuhusu kupata mglu6iyagonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.
Ingawa kutofanya mapenzi kabisa ndio njia pekee ya uhakika ya kuepuka maambukizi ya VVU, watu wengi hawajui kwamba kuna magonjwa mengine ambayo unaweza kupata maambukizi ya bila hata kufanya mapenzi.
Maambukizi ya mfumo wa mkojo ni tatizo kubwa sana. Yanasababisha maumivu makali na yasiyoisha. Je, umegundua kuwa mara zote ulizogundua umepata maambukizi ni baada ya kutoka kufanya mapenzi? Gazeti la New York Times limeripoti utafiti unaoonesha kuwa asilimia 80 za maambukizi ya UTI yanatokea ndani ya saa 24 tangu kufanya mapenzi. Ni kawaida kwa mwanamke kupata maambukizi akifanya mapenzi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Hata kipindi cha wiki mbili au tatu kinatajwa kuwa ni muda mrefu kutofanya mapenzi, kwahiyo, kwa wanawake kuwa mbali na wapenzi wao kwa muda kunawaweka kwenye hatari ya kupata UTI.
Faida pekee unayopata kwa kutofanya mapenzi muda mrefu ni kwamba unakuwa na hakika nani aliyekuambukiza, lakini ukianza tena kufanya mapenzi mara kwa mara, ni kama una uhakika wa asilimia kubwa kwamba upo mbioni kupata maambukizi. Ni kama mshale wenye ncha mbili, ya faida na hasara.
8. Kusahau mara kwa mara

Uwezo wa kiakili unapungua. Kusahau mara kwa mara ni tatizo kubwa ambalo mwanamke anapata asipofanya mapenzi mara kwa mara kwa sababu hii: Kufanya mapenzi inasaidia kuchangamsha mishipa iliyopo kwenye ubongo inayoitwa hippocampus ambayo kazi yake ni kutawala hisia, kumbukumbu na mfumo wa fahamu, ambayo husaidia sana kuweka kumbukumbu, lakini utambue kwamba haihusiki na kumbukumbu zako zote. Wakati unafanya mapenzi, seli mpya huwa zinatengenezwa kwenye mishipa hii, jambo linalosaidia kwenye kumbukumbu. Unapoacha kwa muda mrefu, kazi hii inakuwa haifanyiki na kusababisha kuzorotesha uwezo wako wa kumbukumbu.m

Thursday 19 July 2018

JINSI YA KUMFURAHISHA MWANAMKE KATIKA MAPENZI

WATU wengi (hasa baadhi ya wanaume) ama hawajui au hawajali ni kitu gani wenza/mwenza wake anataka kufanyiwa au akifanyiwa kitamsisimua (Turn on) hata kama amechoka sana.
Uchunguzi unaonyesha kuwa Wanaume wengi hasa kutoka nchi za Kiafrika hujali zaidi kumaliza hamu zao za mwili na kamwe hawajali kama wenza/Mwenza wake yuko tayari au la!.
Mf: Inasemekama baadhi ya Wanaume wa Kiafrika ambao ni wakubwa kiumri (wa zamani), au wale ambao wanathamini sana jadi zao asilia ndani ya Afrika, kitu cha kwanza watakacho kuambia mkiwa chumbani ni "njoo hapa" au "vua nguo basi" na kisha utavamiwa kabla hata wewe mwenyewe hujawa tayari na unalazwa chini kama sio unawekewa uume mbele ya uso wako.......halafu watu mnashangaa kuambiwa "mume wangu alinibaka".
Mfano huo unaonyesha ni kwa jinsi gani baadhi ya wanaume wanavyojipendelea(wabinafsi), na mara zote huweka akilini mwao kuwa wanawake/mwanamke ni chombo cha kumridhisha / kumstarehesha/ kumfurahisha na kumliwaza yeye "mwanaume".
Napenda kusema kuwa mwanamke kama mwanadamu pia anahaki ya kuridhishwa, kustareheshwa, kufurahishwa na kuliwazwa pia.

Dhana hiyo potofu imepelekea baadhi ya makabila kuendeleza mila za kuwakusanya wasichana ktk umri wa kuvunja ungo (mwali) na kuwafundisha jinsi ya kuwaridhisha mwanaume kimapenzi " hao wana bahati".
Lakini kwa wale ambao hawafuati/hawana/hawazijui mila hizo wamekuwa wakifuatilia kwa makini na kuamini kila kinachoonyeshwa kwenye "Video" ailimradi tu kiwe kinahusu jinsi ya kumridhisha mwanaume kimapenzi.

Inasikitisha sana kuona pia baadhi hufuatilia hatua kwa hatua kila kinachoandikwa kwenye Magazeti na baadhi yao huamua kutafuta "Kungwi" na kulipishwa ili wapatiwe ujuzi wa kufanya mapenzi ili kuwaridhisha wapenzi wao.
Ninavyofahamu mimi ni kuwa , ujuzi, utundu katika kufanya mapenzi haufundishwi hata kidogo ila ni
-ubunifu wako,
-kujaribu,
-kuujua mwili wako na wa mpenzi wako,
-ufurahiaji wa mwili wako,
-kujiamini kwako,
-uwazi na ushirikiano wa mpenzi wako.
Ni vema jadi ikabadilishwa na swala zima la kufundishwa/fundwa liwe kwa jinsia zote mbili. Wake kwa waume wafundishe jinsi ya kuridhishana, jinsi ya kufurahia na yale mambo muhimu ya mahusiano ya kimapenzi iwe ni ndoa au mahusiano ya kudumu nje ya ndoa.
Pia ni vizuri utambue kuwa unapoamua kufanya tendo la Ndoa au Ngono ni vyema ukajua mahitaji ya mwenzio iwe mwanaume/mwanamke, jaribu kufamnyia Mwenza wako kitu/vitu tofauti na alivyokuwa akitarajia/alivyozoea ni vizuri zaidi na kutamfanya aendelee kuwa na hamu ya kuwa na wewe kwa muda mrefu "usipigwe kibuti" kwa vile unamjulia.....yaani unajua vipele vilipo na unavikuna vilivyo.

Monday 18 June 2018

FAIDA ZA KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA UJAUZITO

kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito? maswali yalikua mengi sana hivyo leo nimeamua nijibu maswali hayo na makala hii.

mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi ambazo ni muhumu kiafya.faida zenyewe ni kama zifuatazo
husaidia uchungu mzuri na kupona mapema; kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.
hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea; wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.

huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba; tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.

hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida; kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.
huwapa uwezo wa kujiamini ; kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.

hupunguza msongo wa mawazo ; kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je ntapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin, homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.

huongeza upendo na mshikamano kati ya wapenzi; katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana.

hukuandaa na uchungu ; ukishiriki ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.

hutibu tatizo la kukosa usingizi; wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri.

hupunguza presha ya damu; kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.

mwisho; hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa, kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, mwanamke kuja juu, au mwanamke kuinama

Sunday 17 June 2018

UJUMBE MUHIMU KWA WAKINA DADA/ WANAWAKE


DEAR LADIES


1 . Ngono haimfanyi mwanaume asikuache , hata ukukuruke vipi , jikwatue kiasi gani kama hajaona quality za kuwa mke atakuacha tu .

2 . Mwanaume anaekupata kwa vile alitumia pesa zake kwako hatakaa na wewe milele . Wanaume halisi hawawezi wakatoka na wanawake feki wanaopenda pesa. Ukibahatika sana atakufanya daraja la pili yaani mchepuko!

3 . Uzuri wa mwanamke unaweza ukampelekea akaolewa ila tabia yake ndio itakayoamua ni kwa muda gani atadumu katika ndoa. Uzuri huvutia wanaume, ila tabia hufanya wanaume wadumu na wewe.

4 . Pesa kiukweli ina faida sana na ni muhimu kwa mtu yoyote kuwa nayo ila pesa peke yake haiwezi kuleta ukweli wa maana halisi ya furaha na maisha .

6 . Kuwa mzuri bila tabia njema hakuwezi kukakupa mume bora, sana sana utapata Boyfriends na wanaume za watu .

6 . Tendo la ngono linaleta faraja ila haliwezi kuleta upendo. Sex ni zao la mapenzi, mapenzi sio zao la sex .7 . Sex inaweza kufanya mwanaume alale na wewe usiku kucha, na asubuhi akaondoka zake ila upendo hufanya mwanaume aishi na wewe daima.

8 . Kuna mambo mengine pesa haiwezi nunua kama tabia na heshima, kama ulikubali kuolewa nae kisa pesa zake . Usidhani kupitia pesa zake ataweza badilika.

9 . Uvaaji wako siku zote ndio utakaoamua ni nini wanaume wazungumze na wewe!
Ni ukweli fulani hivi ambao ni mchungu ! ila sio mbaya waweza shushia na juice bariiiiiii

Saturday 16 June 2018

MWANAMKE KUWA JUU YA MWANAUME NI MTINDO HATARI KTK TENDO LA NDOA

Wanasayansi nchini Brazil wamefanya utafiti ili kubaini ni mtindo upi katika ufanyaji tendo la ndoa ulio hatari zaidi kwa mwanaume.
Kwa mujibu wa utafiti huo, mtindo ambao mwanamke anakuwa juu ya mwanaume ndio hatari zaidi na huwa na risk kubwa zaidi ya kusababisha hata kuvunjika kwa uume.
Wanasayansi hao wanasema:
Pindi mwanamke anapokuwa juu, mara zote hucontrol movement na uzito wote wa mwili wake ukitua kwenye uume uliosimama na kushindwa kuzuia pale uume unapokuwa umeingia vibaya kwasababu madhara huwa ni madogo kwa mwanamke bila maumivu lakini ni mabaya kwa mwanaume.
“Pindi mwanaume anapokuwa akicontrol movement, ana nafasi kubwa ya kuzuia kutokana na uume wake kuwa sehemu mbaya na hali inayopelekea kusikia maumivu na hivyo kupunguza hatari.
Hivyo inashauriwa kuepuka staili hiyo....

Tuesday 12 June 2018

MADHARA YA KUZAMA CHUMVINI KWA MWANAMKE

Tafiti zimeonyesha kuwa,mdomo wa binadamu ki bacteriologia (bacteriologically) ni mchafu maradufu kuliko sehemu ya uke(vagina).

Ni vema kufahamu kuwa,katika hali ya afya,binadamu wote tunaishi navimelea(microorganisms) katika sehemu nmbalimbali za miili yetu, wakiwa na lengo la kutulinda, kitaalamu wanaita normal flora hawa wanakuwa hawana madhara katika mwili.Hivyo ni kweli kuwa vagina kama ilivyo mdomo una normal flora.

sasa baadha ya vitendo huweza kuondoa normal flora na kukaribisha magonjwa,mfano kinamama kujiosha ukeni na maji ya ndimu,limao,Shabu etc huweza kuondoa Normal flora na kukaribisha magonjwa,kama ambavyo matumizi ya sabuni zenye kemikali zinavoweza kuua normal flora kwenye ngozi na kusababusha magonjwa ya ngozi.Hivyo kwa mwanamke mwenye afya,uke ni mahali salama kufanya upendalo(kama vile kwenda chumvini).

Hata hivyo, nionye kuwa hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa kinywani kama vile Gonnorhea, Syphilis, candidiasis (fungus), HIV n.k ipo pale pale kama ambavyo mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya kawaida ya kujamiiana.

Mwisho, kama wewe ni mgonjwa wa kwenda chumvini, hakikisha unafanya mchezo huo nampenzi/mke aliye salama.