Sunday 17 June 2018

UJUMBE MUHIMU KWA WAKINA DADA/ WANAWAKE


DEAR LADIES


1 . Ngono haimfanyi mwanaume asikuache , hata ukukuruke vipi , jikwatue kiasi gani kama hajaona quality za kuwa mke atakuacha tu .

2 . Mwanaume anaekupata kwa vile alitumia pesa zake kwako hatakaa na wewe milele . Wanaume halisi hawawezi wakatoka na wanawake feki wanaopenda pesa. Ukibahatika sana atakufanya daraja la pili yaani mchepuko!

3 . Uzuri wa mwanamke unaweza ukampelekea akaolewa ila tabia yake ndio itakayoamua ni kwa muda gani atadumu katika ndoa. Uzuri huvutia wanaume, ila tabia hufanya wanaume wadumu na wewe.

4 . Pesa kiukweli ina faida sana na ni muhimu kwa mtu yoyote kuwa nayo ila pesa peke yake haiwezi kuleta ukweli wa maana halisi ya furaha na maisha .

6 . Kuwa mzuri bila tabia njema hakuwezi kukakupa mume bora, sana sana utapata Boyfriends na wanaume za watu .

6 . Tendo la ngono linaleta faraja ila haliwezi kuleta upendo. Sex ni zao la mapenzi, mapenzi sio zao la sex .7 . Sex inaweza kufanya mwanaume alale na wewe usiku kucha, na asubuhi akaondoka zake ila upendo hufanya mwanaume aishi na wewe daima.

8 . Kuna mambo mengine pesa haiwezi nunua kama tabia na heshima, kama ulikubali kuolewa nae kisa pesa zake . Usidhani kupitia pesa zake ataweza badilika.

9 . Uvaaji wako siku zote ndio utakaoamua ni nini wanaume wazungumze na wewe!
Ni ukweli fulani hivi ambao ni mchungu ! ila sio mbaya waweza shushia na juice bariiiiiii

No comments:

Post a Comment