Kuna sheria ndogo ndogo na taratibu ambazo kiumeni.com itakupa zinabidi zifuatwe ili kukuongezea wigo wa uhakika wa kumpata msichana facebook, na iwapo ukizingatia vizuri na ukaweka umakini utashangazwa na mabadiliko utakayotokewa na kuyaona...
USIMTUMIE MWALIKO WA URAFIKI MAPEMA MNO...
Wapo wanaume wengi wanaomtumia mialiko mingi ya kumuomba urafiki, kwa hio hakikisha usiwe mmoja wao, jaribu kutumia njia mbadala kama kukomenti kwenye komenti za marafiki zake anazo zikomenti na yeye, na hakikisha unakomenti kwa utata ili akujibu na tafuta rafiki yake ambae pia ni rafiki yako ili aweze kuwatambulisha, na kama kuna uwezekano wa kukutana nae nje ya facebook ni vizuri ukafanya hivyo kabla ya kutuma mwaliko wa urafiki ili mpate kujuana kwanza, hii itaongeza wigo zaidi na uhakika wa kuwa karibu.
USIMTUMIE POKE...
Kumpoke mtu ambae hakufahamu vizuri mara nyingi huwa haviendani, kwanza huyo msichana atakuona wa ajabu sana mpaka unashindwa kusema "Mambo?" au sana sana anaweza akakupuuzia tu, na tofauti na hapo poke inauwa chachu ya kuanzisha mazungumzo.
USIJISHUSHE NA KUONEKANA MPUMBAVU..
Kama hakujibu meseji na chati zako ulizotuma kabla au komenti ulizoziacha kwenye kuta za kurasa yake ya facebook, ni vizuri ukamwacha kwanza mpaka akujibu mwenyewe.
FIKIRIA KAMA VILE KILA MTU ANAMJUA KUWA YUPO FACEBOOK..
Hapa tunamaanisha kila mtu, bibi yake, bosi wake, mwalimu wake, mama yake, hii inamaanisha usiandike kwenye kuta wa kurasa yake mambo ambayo hayaendani au usimwoganishe jina lake kwenye picha ambayo haina muonekano mzuri, iwapo ukimdhalilisha mbele ya jamii yake sidhani kama utakua na nafasi tena kumpata.
KUWA MWENYE UHARISIA..
Sio kwa sababu ulishamchunguza kwenye kurasa yake na kugundua anachopendelea na wewe ukajifanya una hobi hizo hizo na kuwa wa kwanza kuvisema kwake, ukifanya hivyo utaharibu, ni vizuri ukamuuliza au mwache mwenyewe mpaka atakapokuambia kwa maneno yake
TOA UHUSIANO KWENYE MTANDAO..
Baada ya muda ni vizuri utoe uhusiano kwenye mtandao na uende nje ya facebook na kukutana ana kwa ana, iwapo ukitumia muda mwingi wa mawasiliano kwa njia ya mtandao, itakua ngumu kuuleta uhusiano katika hali ya kawaida ya kidunia.
No comments:
Post a Comment