Mwanamuziki mkongwe wa hip hop na Mbunge wa Mikumi, professa Jay, amefunguka juu ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kufungia wasanii na baadhi ya kazi zao.
Jay amesema BASATA wanapaswa kukaa na wasanii na kuzungumza nao, ikiwezekana kutoa semina elekezi, lakini sio kuwafungia kwani wasanii wanapitia mengi magumu kwenye kutengeneza kazi zao.
Amesema kuwa “Unajua asilimia kubwa ya taifa ni vijana, na wengi wao wanajishughulisha na sanaa mbali mbali, suala la kufungiwa huu muziki tumetoka nao mbali sana, mtoto akikosea usimchinje kichwa, tujaribu kufanya semina elekezi, kumfungia mtu kama roma ni kitu kikubwa, hii inarudisha nyuma na inakatisa tamaa”.
Prof Jay ameendelea kwa kusema kwamba yeye kama muwakilishi wa wananchi na wasanii pia, atalisemea hili bila kuchoka.
Sunday, 25 March 2018
Basata wazidi katolewa akili -pr_jay
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment