Saturday, 10 February 2018

Simon msuva Apiga Hart-tric

Simon Msuva ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Difaa Hassani Eljadida ya nchini Morocco, leo Jumamosi Februari 10, 2018 ameingia kwenye vitabu vya historia baada ya kupasia nyavu mara tatu ‘hat-trick’ katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Benfica Bissau.
Msuva akicheza mchezo wake wa kwanza wa mashindano ya afrika akiwa na klabu hiyo ameisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 10-0 kwenye uwanja wa nyumbani ukiwa ni mchezo wa awali kabla ya timu hizo kurudiana katika mchezo wa marudiano.
Katika mchezo huo, Msuva amehusika katika magoli sita (amefunga magoli matatu na kutoa pasi tatu zilizo zaa magoli)  huo ni mwanzo mzuri kwa Msuva ambaye pia anafanya vizuri katika ligi ya Morocco tangu alipojiunga na Difaa Hassani el Jadida.
Magoli mengine yamefungwa na Hamid Ahdad ambaye amefunga magoli matano, huku magoli mengine mawili yakifungwa na Bilal el Magri pamoja Bakary N’diaye

No comments:

Post a Comment