Saturday 24 February 2018

NIMEJIFUNZA JAPOKUWA NIMEUMIA SAANA?! Diamond... Sikutegemea

NIMEJIFUNZA JAPO NIMEUMIA SANA PIA
Nilijitoa kuwa mke mwema na mama bora wa watoto wako, nikaepuka skendo na kashfa kukulindia heshima yako kama mume wangu wa maisha ila nasikitika nilikua napoteza muda tu, hukujali yote hayo umenisaliti mbaya zaidi hadharani hadi kuzaa na wanawake ninaowajua waliokuwa marafiki wa familia yetu waliokuwa wanakuja kushiriki tafrija mbalimbali nyumbani kwetu kumbe wana njama mbadala na wewe hukujali ulijua ukaacha wanichore, nasikitika sana hukujali maumivu makali ambayo ningeyapata siku nitayojua.
NIMEJIFUNZA JAPO NIMEUMIA SANA
................ Maisha ndivyo yalivyo, waeza mpenda mtu na kumpa dhamana ya moyo wako wote ila kumbe mwenzio moyo wake kashampa mtu mwingine, mwishowe mnaachana hapo ndipo wewe uliependa kweli utapoisoma namba wakati yeye atabaki na tabasamu kwa kuwa wala hata haukuwa moyoni mwake kama ulivyokua ukifikiri, ulijua umepata kumbe umepatikana, hupendwi kwa dhati, ulikua wa kuzugia tu. Ikitokea uhusiano huo umevunjika na mkaaachana usijute wala kusikitika bali chukua nafasi jipe mda Tafakari ujiridhishe nini chanzo na mwelekeo mpya wa barabara usijeangusha gari tena.
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda..

No comments:

Post a Comment